WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Thursday, April 4, 2013

MSANII WA FILAMU JIJINI ARUSHA AIBUKIA KWENYE MUZIKI WA HIP HOP

Msanii Ray Swing aliyechuchumaa



Msanii wa siku nyingi katika tasnia ya filamu hapa Jijini Arusha ambaye alivuma ipasavyo kwenye filamu ya MATEKA WA KIROHO na kuiwakilisha vyema Jiji la Arusha katika tasnia hiyo ameamua kuingia kwenye muziki wa hip hop.
Msanii huyu anafahamika kwa jina la RAYMOND NGADA a.k.a Ray swing kama anavyojulikana kwenye tasnia ya muziki huo wa kizazi kipya amesema kua wasanii wa hip hop wakae chonjo kwani yeye ni moto wa kuotea mbali.


Hata hivyo hivi karibuni mwandishi wa blog hii alifanikiwa kumuona msanii Ray swing akitumbuiza katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA akiimba wimbo wake uliobeba jina la album ya JEMEDARI na wimbo huo ukionekana kumsifia Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Gobless Lema na Katibu Mkuu wa CHADEMA Bwana Wilbroad Slaa.


Msanii huyo anayetokea kundi la sanaa la AGESTA ameamua kuingia kwenye muziki kwa sababu ana vipaji vingi na muziki nao ni moja ya kipaji chake alichotunikiwa na Mwenyezi Mungu ili kuiburudisha na kuielimisha jamii.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii msanii huyo amesema ameamua kuachia album yake ya kwanza inayofahamika kwa jina la JEMEDARI na ameamua kuisambaza bure kabisa kwa watanzania wote na hadi sasa ameshasambaza nakala zaidi ya 400 kwa mashabiki wake.
Aidha alipoulizwa kuwa kilichosababisha yeye kuingia kwenye muziki wa hip hop ni kutokana na yeye kuchuja katika tasnia ya filamu  alisema kuwa ameamua kufanya sanaa ya filamu na muziki kwani vyote anaviweza na anaamini vitamuingizia kipato na kumnyanyua kimaisha.
Ukitaka kumsikiliza au ku-download nyimbo zake zote za album ya JEMEDARI unaweza kuipata bure kabisa kwa kutembelea www.nellykivuyo.blogspot.com sasa ili umpe-support msanii huyu.

No comments:

Post a Comment