WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Monday, February 25, 2013

NGONO ZEMBE YAVURUGA KAMBI YA WASANII

KASSIM a.k.a KIM


Katika hali isiyokuwa ya kawaida na yakushangaza,wasanii wa filamu waliokuwa wameweka kambi kwaajili ya kurekodi filamu ambayo bado haijapewa jina kamili,wakiwa katika maeneo ya Esso jijini Arusha,wamejikuta katika hali yamdomo wazi baada ya kutimuliwa katika kambi hiyo hivi karibuni kwa kile kinachodaiwa kukithiri kwa vitendo vya ngono ndani ya kambi hiyo.

Kwa habari kamili zilizofikia meza ya habari ya blog hii na kuzibitishwa na mwenyekiti wa shirikisho la sanaa ya filamu jiji la Arusha Bw.Kassim maarufu kwa jina la Kim,zilidai kuwa kambi hiyo ilikuwa inatia kichefuchefu na kukosa maadili ya sanaa.

“Ndugu mwandishi yani huwezi kuamini,mimi nilipata habari hizi kupitia mmoja wa wasanii na ikanilazimu kama kiongozi niende katika hiyo kambi iliyokuwa maeneo ya Eso nakushuhudia madudu hayo ,kama mwenyekiti niliamua kuivunja na kuwatimua wasanii wote na kuwaambia kama wataendelea nitaita polisi,sasa cha kushangaza aliyekuwa anaongoza kambi hiyo ni kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika shirikisho(jina kapuni)”.alinukuliwa Bw.Kim akisema.
Baada ya kubanwa kwa muda mwenyekiti aliamua kufunguka juu ya kiongozi huyo kuwa ni katibu wa shirikisho hilo Bw.Isack ambaye inasemekana amejiuzuru katika wazfa huo baada ya mtafaruku baina ya viongozi kisa pesa.

Aidha wasanii hao walidaiwa kukesha kambini hapo huku kila mtu akiwa na mwenza wake ndani ya wasanii hao hao na hata muda mwingine kubadilishana bila hata uwoga  wala aibu.
Kwa niaba ya wanasanaa,dawati la habari la blog hii linawaomba wasanii kujiheshimu na pia kwa wale ambao wanavamia sanaa na kuitia doa kuacha kwani sanaa ni kazi na si mahali pakufanyia uhuni.

No comments:

Post a Comment