WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Friday, February 8, 2013

STAA WA FILAMU YA STANDARD 7 AKIMBIA CLASS.




MWANAHAMISI MZIRAY a.k.a MISHI
Mwanadada machachari aliyeuza sura nakufanya vema katika filamu bomba ya Standard 7 Mwanahamisi Mziray kwa jina maalufu “Mishi” ametimiza usemi wa filamu hiyo baada ya kukimbia kupiga kitabu katika vyuo viwili tofauti mkoani hapa.


Mrembo huyo alikuwa akipiga darasa katika chuo cha Sila huku akisoma ishu za mapishi nakujikuta akiingia katika kisanga hicho baada yakunogewa na uuzaji sura .
Hata hivyo baada ya kumaliza filamu hiyo alipata shavu kubwa  lingine lakuigiza filamu iliyotumia lugha yakimombo nakujikuta akitupilia  mbali ishu ya kupika na kukimbilia katika chuo maarufu cha lugha jina tunalihifadhi nakuanza kujifunza lugha hiyo.
Aidha alijikuta katika wakati mgumu baada ya muda aliopewa na waandaaji wa filamu hiyo toka nchini Kenya kuisha huku kimombo kikiwa bado cha yes/no??!!”? ,hali iliyopelekea msanii huyo kukimbia tena daftali nakufanya filamu zenye lugha ya Kiswahili.
Baada yakupoteza bahati hiyo,alipotezea ishu za kitabu nakuamua kulandalanda akisaka filamu za kucheza kujiwekea jina hata kama ni bure jambo ambalo lilizidi kumpoteza kabisa katika tasnia hiyo licha yakufanya vema katika filamu ya standard 7.
Baada ya kudakishwa kwa stori hii,blog hii ilimlushia waya Mishi naye alikiri kukimbia kitabu lakini si kwakutopenda kitabu bali mikataba mingi ya kucheza filamu ndani na nje ya Arusha hivyo hali hiyo kumpa ugumu wakutulia kusoma labda kwa baadae sana.

MISHI

No comments:

Post a Comment