WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Wednesday, February 6, 2013

FUMANIZI LA MWAKA

DJ ANGWISA
Hii ni kali na haijawahi kutokea hapa Jijini Arusha, hii ni baada ya mtangazaji maarufu Tanzania na msanii wa filamu kufumaniwa akiwa katika hoteli moja maarufu hapa jijini Arusha.
Mtangazaji huyu aliyetangaza kwenye vyombo mbalimbali hapa Tanzania kama RADIO 5, SUNRISE RADIO za Arusha na RADIO VISION iliyoko Bukoba pamoja na kucheza kwenye filamu na tamthilia nyingi kama MATEKA WA KIROHO, STANDARD 7, CHOZI LA YATIMA na mzigo ngáda uitwao TEMPTETION OF MY WIFE utakaoshuka hivi karibuni toka STEPS ENTERTAINMENT pamoja na tamthilia ya HAIBA YA PENZI, inasemekana kuwa aliamua kufanya hivyo baada ya kuachana na aliyekua mchumba wake (jina kapuni)
Fumanizi hili la msanii huyu maarufu wa filamu na mtangazaji mkongwe wa siku nyingi ndugu SEVERINUS MWIJAGE Jr a.k.a DJ ANGWISA ilitokea katika hoteli maarufu hapa jijini Arusha ya SNOW CREST iliyopo maeneo ya ngulelo.
Inasadikika kuwa huyu ni msichana wa nne kuwa nae baada ya kuachana na aliyekua mchumba wake hapo mwanzoni mwa mwaka huu.

MWIJAGE NA ALIYEFUMANIWA NAYE
Kama kawaida yetu lazima story iwe balanced tuliamua kumtafuta ndugu yetu Severinus Mwijage Jr ili athibitishe tuhuma hizi kuwa ni za kweli au ni uzushi naye akafunguka kama ifuatavyo “ Ni kweli nilikua snow crest na huyu binti tulikutana naye hapo kwani nilikua narekodi kipindi cha THE YOUNG MILLIONAIRE ambacho ni kipindi kipya cha ujasiriamali kitakachokua kinaoneshwa kupitia moja ya runinga hapa Tanzania”
Alipoambiwa atoe maelezo zaidi hakutaka na kusema ni hayo tu….
Lakini kwa habari za uhakika ni kwamba muda aliofumaniwa ilikua ni saa nne za usiku na hakukua na crew yoyote ya kurekodi kipindi chochote kile…
www.arushaprofessionalmovies.blogspot.com itamtafuta aliyekua mchumba wa ndugu Severinus Mwijage naye atoe yake ya moyoni.

No comments:

Post a Comment