WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Tuesday, March 19, 2013

BAADA YA KUKIMBIA DARASA NA KUIBUKIA KATIKA TASNIA YA FILAMU. FIGA MAUZO YAJIKUTA YAANGUKIA KATIKA UPISHI WA CHAKULA KATIKA KAMBI YA WASANII.



Baada ya kuanikwa wazi juu ya kukimbia darasa kwa mrembo mwenye figa matata  katika tasnia ya filamu jijini Arusha  Mwanahamisi Mziray (Mishi),bidada huyo amejikuta akizidi kuangukia pua baada ya mambo katika tasnia hiyo kuzidi kumuendea vibaya na kujikuta akiwapikia wenzake chakula katika kambi waliokuwa wameweka kabla ya kuanza kupiga kizigo cha filamu yenye utata hadi hivi sasa.
Bishosti huyo alieonekana kuja kwa kasi katika tasnia hii akiamini ni njia rahisi zaidi ya kutokea mambo yamezidi kumuendea ndivyo sivyo nakujikuta akitapatapa katika vikundi.


Chanzo chetu makini kilitupitishia kavu kavu kuwa bidada Mishi baada ya kuanza vyema kwa kucheza katika filamu ya Standard 7 alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuibuka kwa shosti mwingine katika kampuni aliyoanza nayo nakufunikwa katika uchezaji,jambo lililomfanya ahame kampuni nakuanza kusaka vikundi vya sanaa.
Hata hivyo kama ulivyo msemo wa maisha ni popote,Mishi aliamua kutumia swaga hizo na kuanza kusaka sanaa kona hadi kona akiambulia kucheza filamu zisizo isha na kujikuta katika kambi ya kundi la OSG lililokuwa likijianda na kucheza filamu nayeye kujikuta akipewa kazi yakuwapikia wasanii wenzake hata hivyo alifanya akiamini atapata nafasi yakucheza filamu.
Aidha msemo wa kifo cha nyani miti yote kuteleza nao ukadhihilika wazi baada ya bidii yote ya kuwapikia wenzake akisaka nafasi kutokana na wasanii kuwa wengi,kambi hiyo ilivunjwa mara kwa mara kutokana na sababu tofautitofauti ikiwemo ngono nzembe baina ya wasanii nakupelekea kufukuzwa nawahusika wa maeneo waliokuwa wanaweka kambi.
Baada ya kashkash hizo,hakuonekana kukata tamaa akijaribu kusikiza msemo wa penYe nia pana njia lakini mambo hayajaonekana kuwa sawia,hata hivyo blog hii ilizungumza na baadhi ya wasanii wenzake waliokuwa nae kampuni kipindi cha filamu ya standard 7 na kumshauri bidada huyo kutokuogopa chalenji hivyo arudi atulie katika kampuni kwani anazidi kuchuja na kupotea kabisa katika tasnia ya filamu.

BAADA YA KIPIGO KITAKATIFU CHA MAGOLI 6 KWENDA RADIO5, KUNDI LA SANAA OSG KUNUSA 5.


 JUMAMOSI HII WABABE WA SOKA KAMPUNI YA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT DIMBANI  TENA.

Baada ya mechi mfululizo za kujiweka fiti kiafya na kudumisha urafiki baina ya makampuni na vikundi vya sanaa jijini Arusha ,kampuni inayokuwa gumzo mjini Arusha kwa kazi safi za filamu pamoja na kusakata kabumbu,jumamosi hii tena kuumana na kundi la sanaa la AYSAG la mjini hapa katika uwanja wa shule ya msingi meru walio na hamu ya kuonja shubiri ya magoli.


Akizungumza na blog hii mkurugenzi wa kampuni babkubwa ya filamu jijini hapa Bw : Elias Magesa ambaye pia ni straika matata afungae dakika za lala salama na kuzua kilio kwa timu pinzani alisema kampuni yake iko fiti kwa mchezo kwani licha ya mazoezi ya sanaa kila siku huanza na mazoezi ya viungo jambo linalowaweka katika ubora kimwili nakuwa tishio katika makampuni na vikundi vya sanaa.
Hata hivyo amewaomba wasanii wa AYSAG kujipanga vema nakufanya mchezo wa kiungwana kwa lengo la umoja wavikundi na sio kuweka mamluki kama walivyo fanya kundi la OSG kwani si lengo la kisanaa na mchezo kwa ujumla,pia aliomba wadada wa kundi hilo kujitokeza kucheza pia ili soka kuwa nzuri na yenye kuvutia kwa lengo la furaha.


Nae mkurugenzi wa kundi la AYSAG Bw: Kim alisema wapo tayari kwa mchezo huo na kuahidi kuweka wadada ili kuwafanya wasanii wote kushiriki vema katika mchezo huo kwani hakutakuwa na mchezo wa pete nakuahidi mchezo wakiungwana na furaha akisema wanajua maana ya michezo na sanaa.

Nae Kapteni wa timu ya Kampuni ya Emags Ibrahim Jamal amewaomba wasanii wote kuwahi uwanjani ili kuanza mapema na kuhitimisha kwa furaha za kisanaa,akitoa angalizo la AYSAG kuwa makini kwani wataondoka na kapu la mabao na kuomba wadau kujitokeza kushuhudia kandanda safi.
Aidha blog hii inawatakia mchezo mwema na wenye furan a amani na pia kuahidi kuwapa wasomaji matokeo kila baada ya dakika ya mchezo huo.

Tuesday, March 12, 2013

BINTI ATUMIA MBINU ZA KI-ANALOJIA KURUDISHA MAPENZI YAKE KWA MSANII WA FILAMU


-Amnunulia lunch kwa kumrubuni

MPENZI WA MWIJAGE WA ZAMANI
Lile sakata liliosababisha msanii wa filamu hapa Jijini Arusha kutoka kimapenzi na wasichana tofauti tofauti limechukua sura mpya baada ya mpenzi wake aliyemsababishia hiyo hali kutaka kurudisha mahusiano yao ya awali.

SEVERINUS MWIJAGE Jr
Blog hii imepata taarifa hizi kupitia msanii huyo ambaye alifunguka baada ya taarifa hizi kufikia chumba chetu cha habari mapema jana mchana majira ya saa saba.
“Ni kweli ndugu mwandishi jana majira ya saa saba mchana nilipokea simu kutoka kwa mpenzi wangu wa zamani ambaye alisema anataka kuzungumza nikamkubalia kwa kuwa sina ugomvi nae” alisema msanii huyo.

MWIJAGE NA MPENZI WAKE ENZI ZA MAPENZI YAO
Msanii huyo anayefahamika kwa jina laSeverinus  Mwijage Jr maarufu kama Dj Angwisa aliendelea kufunguka kuwa “ Binti huyo baada ya kutaka kukutana na mimi alinipeleka kwenye moja ya mgahawa hapa Mjini akaninunulia chakula cha mchana kwa lengo la kutaka kunishawishi ili nirudiane nae”

HAPA WALIKUA MOJA YA FUKWE HAPA NCHINI
Habari za uhakika zilizopatikana zinasema kuwa binti huyo kwa sasa anahangaika kila kukicha kutafuta ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa Mwijage ili waweze kumshawishi kurudisha uhusiano wao wa mwanzo.

MAPENZI YALIKUA MOTOMOTO KWELI ENZI HIZO
Rafiki wa karibu wa ndugu Mwijage aliweza kutupenyezea habari kuwa majira hayo ya mchana binti huyo alionekana nyumbani kwa Mwijage akilazimisha uhusiano wao kurudia kama zamani lakini ndugu Mwijage alikua na msimamo kuwa hamtaki na hayo mambo kwa sasa yanazungumzwa kifamilia.


NANI ALIJUA KUWA WATAGOMBANA?
Endelea kutembelea blog hii ili tukuhabarishe kitakachoendelea baada ya familia hizi mbili kuzungumza na binti huyu kuendelea kutafuta muafaka wa penzi lake kwa Mwijage.

MUIGIZAJI WA KIUME ADAIWA KUMTESA MPENZI WAKE : NI BINTI ALIYEANZISHA KANISA LA MIRACLE


 Mcheza filamu na mwandishi wa habari jijini Arusha anayesifika kwa kupenda mauzo atambulikae kwa jina la Deogratius anadaiwa kumtesa mpenzi wake kimapenzi na kumsababishia  baadhi ya makovu mwilini akijiumiza kwa kusudi kwa imani ya kupunguza hasira.


Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa bidada huyo ambaye ni mchungaji wa kanisa la Miracle alilofungua baada ya kutemana na mzigo wa kuuza sura yaani muigizaji (jina kapuni),alidai kuwa shosti huyo kwa sasa anashindwa hata kufanya shughuli nyingine kisa kulilia penzi la HB huyo ambaye amekua kama Jaguar na nyimbo ya kigeugeu.



“mimi namshangaa sana rafiki yangu huyu,ni mwaka na miezi hivi sasa anamngángánia huyu jamaa sijui karogwa?sasa alisema kaacha mambo ya dunia nakuanzisha hadi kanisa ndugu mwandishi wewe ni shahidi ulikuwepo kipindi kanisa laanzishwa,mimi nimemshauri sana basi hata atafute mume lakini hasikii,kafa kaoza kwa huyu jamaa kweli nimewahi kupenda lakini huyu rafiki yangu kazidi’’alinukuliwa akisema binti huyo.

Hata hivyo nyepesi za chini chini zinadai hali ya shosti huyo kuwa mbaya kwani kuna wakati anaonekana kuvimba macho kama mpiganaji masumbwi kwakushinda ndani akilia kama mtoto mdogo jambo linalo mkra swaiba wake huyo.

Aidha Blog hii ilimtafuta Deo na kuzungumzia ishu hii,hivi ndivyo alivyotiririka, “kaka hayo majungu tu,mimi nampenda sana mpenzi wangu,kwanza wamzungumzia yupi?


Haaaaaaaaaa akajikuta anajishtukia kwani hakujua anayezungumziwa ni yupi kwa wakati huo,nikabaki najiuliza anawangapi?lakini nikampa ufafanuzi akatiririka.

“aha kumbe huyo,kaka mi nampenda sana mpenzi wangu na hivi tunavyozungumza mwezi wa nane namaliza mambo,nafunga nae ndoa we jiandae kula pilau tu”.

Baada ya mazungumzo hayo bidada muolewaji naye alitafutwa na kuulizwa kama alikuwa na taarifa juu ya ndoa hiyo ya mwezi nane, “mh ndoa ya nani tena ndugu yangu mana mi nikama nagundu mahusiano yakawaida yananipa kichefuchefu hiyo ndoa ya wapi labda 2015 nikijaaliwa”.heeeeeee kumbe hata hakuna cha ndoa.

Hata hivyo jamaa huyo ameombwa kuwa muangalifu kwani anamfanya binti huyo kuwa mlevi sana kwa sasa jambo linalowaogopesha wasanii wengine kuwa atakuja kunywa hata sumu.

MWAMUZI MBELEKO KWA KIKUNDI CHA SANAA OSG,EMAGS KAMA ULAYA KABAAAANG!



KIKOSI CHA MAUAJI CHA EMAGS

Wasanii wa filamu kutoka kampuni ya Emags Video Entertainments mwishoni mwa wiki waliwafundisha mamluki wa kikundi cha OSG  soka la kiulaya na kuwaacha mashabiki wakinongóna wakiifananisha timu hiyo na timu za ligi kuu bara, na zile za ulaya kwa kiwango walicho kionesha.

IBRAHIM JAMAL AKIINGIA UWANJANI

RODGERS AKIWAITA WACHEZAJI KUFANYA WARM UP

Mechi hiyo iliyokuwa imejaa kila aina ya mbwembwe za kisanii na majigambo toka kwa viongozi na mashabiki wa timu hizo hususani mabinti waliokuwa wamefulika katika kiwanja cha shule ya msingi meru,kilishuhudia kipute hicho kikikamilika kwa pacha ya goli nne kwa nne licha ya kucheza dakika  zaidi ya tisini kwa utashi wa refa aliokuwa akiwatafutia goli OSG waliokuwa nyuma kwa mabao 4 kwa 3 hadi dakika tisini.

Kuonyesha kuegemea upande mmoja mwamuzi wa mchezo huo aligomea goli la tano la Emags baada ya shuti kali lililopigwa na kiungo mchezeshaji wa emags Mau na kumshinda kipa wa OSG na refa kulikataa akidai hakuwa ameruhusu mpira kuanza.

Naye mkurugenzi wa OSG bwana Isack aliyejigamba kushinda mechi hiyo kutokana na kuwa na mamluki wanaocheza ligi ya wilaya Arusha alijikuta akikaa chini baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo,kwani angewalipa fedha mamluki hao pasipokuwa na ushindi.

Aidha upepo ulizidi kuwa mbaya kwao kwani walijikuta wasanii wao wakihamia upande wa Emags na kuanza kuwashabikia mastaa wa filamu toka kampuni hiyo ya Emags  na hata kuomba kupiga nao picha baada ya mchezo jambo ambalo lilimkera bwana Isack na kugomea michezo siku nyingine akidai kuwe na semina za sanaa si michezo kwani haina faida kwao kama kuigiza.

Hata hivyo kila penye wengi hakukosi jambo kwani baada ya mchezo vijana hao waliokuwa wamekodiwa walijikuta wakilipwa pesa chini ya makubaliano nakujikuta wasanii wa osg wakichangishwa tena ili kuondoa aibu ambayo ingetokea mbele ya kadamnasi iliyokuwepo jambo ambalo lilishuhudiwa na paparazzi wa blog hii.

Magoli ya Emags yalifungwa na Maulidi (Mau) -2, Arnold(Dizo),-1  pamoja na kijana mrefu na machachari Aloyce aliyefunga 1 pia,kwa upande wa OSG majina ya wafungaji yalishindikana kupatikana kwania hata mkurugenzi wao hakuwajua majina.

Aidha mchezo ulimalizika bila ugomvi na kufungwa na mkurugenzi wa kampuni ya Emags Bw: Eliasi Magesa aliyetishia amani ya mabeki wa OSG kwa kuwalamba chenga sana na kupiga mashuti makali yaliompa kipa wakati mgumu licha ya umri kuwa mkubwa.naye aliitimisha kwa kuomba michezo iendelezwe ili kuleta urafiki mzuri na pia wasanii kufahamiana ,lakini akiwaomba timu za makampuni ya uma na binafsi ,pamoja na wasanii wa Bongo movie kujipima kwa timu ya Emags kwani iko vema .

Emags ilianza vema kushiriki michezo ilipoitililishia mvua za magoli timu ya Kings Entertainment ya mzee majuto mjini Tanga magoli 9 kwa 2,radio 5 Arusha waliopata kipigo cha bao 6 kwa 1 na OSG waliolazimisha sare kwa kucheza dakika 130 ili kusawazisha

PICHA ZA MATUKIO YA UWANJANI

CAMERAMAN DENNIS ALIKUA AKIFANYA YAKE

BENCHI LA EMAGS WAKIWA WANASHANGILIA

BENCHI LA UFUNDI LA OSG


DIZZLE MAN DILLUNGA AKIPIGA PENALTI

DEO G "GOALKEEPER WA EMAGS"

BENCHI LA EMAGS WAKATI WA MAPUMZIKO

BENCHI LA EMAGS WAKATI WA MAPUMZIKO

EMAGS WAKIFANYA WARM UP KABLA YA MECHI

MAPUMZIKO WACHEZAJI WAKIBADILISHANA MAWAZO

RODGERS, DIZZLE NA MAURICE WAKISHANGILIA GOLI

HEKA HEKA GOLINI MWA OSG

WACHEZAJI WAKIRUDI UWANJANI KUCHEZA KIPINDI CHA PILI

HEKA HEKA ZA UWANJANI

OSG WAKIFANYA WARM UP KABLA YA MECHI

IBRAHIM JAMAL AKIMPA GOALKEEPER DEO G MAZOEZI KABLA YA MECHI

Wednesday, March 6, 2013

BAADA YAKUBUMA JIJINI DAR,MREMBO WA BONGO MOVIE ATIKISA A-city.




Atoa kauli nzito kwa wasanii wa kike “sijachuja,mshikilie uliye nae sichagui kutwa mara tatu”.
Siku chache baada ya kutua katika jiji la Arusha akitokea  jijini Dar mrembo aliyevuma kwa kuharibu ndoa za watu na kutembea na watu maarufu jijini Dar na kufikia hatua yakushindwa kufanya hata sanaa,nakuambulia kuuza sura katika video ya msanii wa muziki jijini aja na jipya jijini Arusha.
Akizungumza na Blog hii msanii huyo aliyefahamika kwa jina la Rose ambaye hivi karibuni aliandikwa na mtandao mwenza na huu baada yakusababisha filamu kushindwa kufanyika akiwagombanisha wasanii waliokuwa wahusika wa filamu hiyo iliyotambulika kwa jina la shadow of pains.
 

Aidha alibainisha kuwa hajachuja hata kidogo na Dar aliondoka baada ya kutamani  kuishi katika mazingira ya baridi kwani alizoea safari za nchi za baridi hivyo bongo kulikuwa kunampa shida na kumuharibu mwili wake uliojazia vema,hata hivyo aliwaonya wasanii wenzake wanaozani amechuja kuwa wawashikilie wanaume zao vema kwani yeye ni zaidi ya kiwembe cha gillete alisema msanii huyo mwenye madoido na jicho la huba.
Licha ya mkwara huo alioingia nao jijini hapa,msanii huyo ambaye anadaiwa kuwa na mahusiano na mtangazaji Jackson John wa kituo maarufu cha radio kinachomilikiwa na mfanyabiashara mkongwe nchini,alijikuta akitulizwa mbwembwe zake na kijana mdogo wa kihaya ambaye ni msanii mwenzake alipokuwa katika mazoezi kwani aliombwa kufanya kipande cha uhusika wa mahaba na kujikuta akihemea juu juu baada ya kuelemewa na ufundi wa chalii huyo mdogo mwenye mambo makubwa na kuzua vicheko kwa wasanii wengine.
Baada ya tukio hilo ndipo minongóno ikaanza kuwa kumbe si lolote si chochote kwani mazoezi yamemnyima pumzi itakuaje katika ukweli,au ndo maana Dar alikuwa anatapatapa nakuachika mara kwa mara,walisikika wenzake wakiulizana.naye hakusita akajibu mapigo kuwa yuko fiti na kuhakikisha hilo atachukua mmoja baada ya mwingine pasipo kujali ni wa nani hata kama mume wa mtu,hata hivyo nyepesi nyepesi nikuwa anataka kuhamia Mwanza kwani Arusha mambo hayalipi kama alivyotarajia.
Kama kawaida ya mtandao huu ,ni kurekebisha tabia hivyo kumuomba dada huyo kutokuaribu tasnia hiyo kwa mkoa huo wala Tanzania kwa ujumla kwani bado mapambano yanaendelea hivyo akafanye kazi nyingine kama sanaa imemshinda…ikumbukwe msanii ni kioo cha jamii na si uhuni.



Friday, March 1, 2013

Msanii azua kashkash kanisa,mchungaji,waumini washikwa bumbuwazi




waumini washika tama wahofu dunia kufikia ukingoni,aibu yamshika msanii atokwa chozi nakujuta.
Mwezi mmoja tu baada ya kanisa la Miracle kufunguliwa na msanii wa kike mjini Arusha aliyeamua kuachana na mambo ya dunia kanisa lake lakumbwa na aibu kama si majaribu toka kwa msanii mwenzake wa zamani aliyeamua kutinga katika kanisa hilo kama mtu aliyeenda katika nyumba ya kawaida kumtembelea rafiki au mtu aendae katika matanuzi kutokana na vazi alilokuwa amevalia.

Ibada ikiwa yaendelea nilipigiwa simu na mmoja wa waumini kuwa katika kanisa kuna jambo la ajabu limejitokeza kwakuwa siko nao mbali fasta nilitoka na kamera yangu mkononi nakwenda kujionea mwenyewe nakupata nyepesi ndipo nilipomkuta binti huyo akiwa kasimama katikati ya kanisa na kumfanya mchungaji kukaa kwa muda baada ya kuona  maajabu ya dunia.

Baada ya muda mzee wa kanisa alionekana akimuomba binti huyo aliyeonekana kutokujali juu ya mavazi aondoke na kwenda kujistiri vema kwani si maadili mema wa nidhamu katika kanisa kwani si sehemu yakihuni,lakini ilionekana kuwa ngumu kwa binti huyo akiamini yuko sawa.

Nao waumini walionekana kuishiwa pozi na wengine walisikika wakisema ama kweli dunia imekwisha kwani huyu binti hana hata chembe ya  aibu?wakati huo mchungaji alionekana kuinama nakuomba na ghafla maombi yakajibiwa baada ya binti huyo kujikuta akitokwa machozi nakuomba kanisa kumsamehe na kumsaidia kwani hakujitambua wala kujua imekuaje alifika katika kanisa wakati alikuwa anaenda katika mambo yake yakawaida.

Baada ya maneno hayo alifunikwa kwa pazia kumsitiri kwani hakukuwa na mwenye kanga na kufanyiwa ibada nakuahidi kuwa muumini mzuri na kuachana na mambo yakidunia.

Msanii huyo  anatamba kwa uchezaji wake wa filamu hivi sasa nakutishia ajira ya mastaa wengi wakike kwa sasa Tanzania.