WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Wednesday, April 3, 2013

VIKUNDI VYA SANAA ARUSHA VYAKUTANA ILI KUUNDA UMOJA WAO

Kutoka kushoto ni Ndugu Ray kutoka kikundi cha AGESTA ambaye alikua katibu wa kikao na upande wa kulia ni Bwana Elias Mages Mkurugenzi wa Emags ambaye ndiye aliyekua Mwenyekiti wa kikao hicho


Viongozi mbalimbali wa vikundi vya sanaa ya Filamu na maigizo Jijini Arusha wamekutana jumatatu ya pasaka kwa ajili ya kutathmini mustakabali wa sanaa ya Jijini Arusha kwa kile wanachoeleza kuwa imekosa mwelekeo.
Blog hii ya Arusha Professional Movies ilishuhudia viongozi mbalimbali wa vikundi vya sanaa wakijadili kwa uchungu sanaa yao ambayo imeonekana kupoteza dira kwa kile  wanachoeleza kuwa waliochangia kudidimiza sanaa hiyo ni viongozi wa shirikisho la sanaa lililoundwa mwaka jana kinyemela.
Mmoja wa wajumbe akitoa maoni yake

Hata hivyo viongozi waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Kampuni ya Emags Video Entertainment maeneo ya Ilboru tank la maji.
Vikundi vilivyohudhuria kikao hicho ni pamoja na AGESTA, NGURUMO YA UPAKO (NYU), FIRE PLACE, KILELE, EMAGS,OSG,GQ FILMS,FICUS,OLERIEN na vingine vingi.

Isack toka OSG naye alitoa maoni yake

Hata hivyo kwa mujibu wa waandaji wa kikao hicho wamesema kuwa walikuwa wamewaalika viongozi wa shirikisho la sanaa Arusha wakiongozwa na mwenyekiti wao Bw Kassim Digiga ila cha kushangaza viongozi hao waliamua kuandaa Bonanza la wasanii wa filamu na waandishi wa habari ili waharibu kikao ambacho kinalenga kuwang’oa madarakani kwa kile kinachodaiwa hamna wanachokifanya kuinua sanaa ya Arusha zaidi ya kujinufaisha wao wenyewe na familia zao.

Mr Hondohondo naye alitoa yake ya moyoni

“Mimi nawashangaa hawa eti wanajiita viongozi wa shirikisho, kwanza hawana elimu yoyote ya uongozi, wengine wanajiita ma-director na ma-producer lakini hawajui hata camera inapigwaje au inashikwaje” hawastahili kutuongoza alisikika kiongozi mmoja wa kikundi ambaye hakupenda atajwe jina lake.
Teacher KT naye alikuwepo katika kikao hicho

Hata hivyo mwingine aliyejitambulisha kwa jina la HondoHondo alisema kuwa “baadhi ya viongozi wa vikundi wanaanzisha vikundi ili wapate wasichana wa kufanya nao ngono”
Kelvin au Abby toka Emags naye alitoa maoni yake katika kikao hicho

Kikao hicho kilijadili kuanzisha chama mbadala cha kuinua sanaa ya Arusha mwelekeo wa sanaa ya Filamu, usambazaji wa kazi za wasanii, ushirikiano wa vikundi na kama kuna uhalali wowote wa shirikisho la sanaa Arusha na kuwaita viongozi hao wa shirikisho ili wawaeleze jinsi walivyoididimiza sanaa ya filamu Jijini Arusha.

PICHA ZA MATUKIO YA KIKAO HIZI HAPA

Fredy, sophia na mwijage pia walikuwepo















1 comment:

  1. Mm n binti wa miaka 22 naishi Arusha mjn napenda filamu sana na napenda kuigiza je ntawezaje kijiunga na vikundi vya filamu please 🙏

    ReplyDelete