WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Tuesday, March 12, 2013

BINTI ATUMIA MBINU ZA KI-ANALOJIA KURUDISHA MAPENZI YAKE KWA MSANII WA FILAMU


-Amnunulia lunch kwa kumrubuni

MPENZI WA MWIJAGE WA ZAMANI
Lile sakata liliosababisha msanii wa filamu hapa Jijini Arusha kutoka kimapenzi na wasichana tofauti tofauti limechukua sura mpya baada ya mpenzi wake aliyemsababishia hiyo hali kutaka kurudisha mahusiano yao ya awali.

SEVERINUS MWIJAGE Jr
Blog hii imepata taarifa hizi kupitia msanii huyo ambaye alifunguka baada ya taarifa hizi kufikia chumba chetu cha habari mapema jana mchana majira ya saa saba.
“Ni kweli ndugu mwandishi jana majira ya saa saba mchana nilipokea simu kutoka kwa mpenzi wangu wa zamani ambaye alisema anataka kuzungumza nikamkubalia kwa kuwa sina ugomvi nae” alisema msanii huyo.

MWIJAGE NA MPENZI WAKE ENZI ZA MAPENZI YAO
Msanii huyo anayefahamika kwa jina laSeverinus  Mwijage Jr maarufu kama Dj Angwisa aliendelea kufunguka kuwa “ Binti huyo baada ya kutaka kukutana na mimi alinipeleka kwenye moja ya mgahawa hapa Mjini akaninunulia chakula cha mchana kwa lengo la kutaka kunishawishi ili nirudiane nae”

HAPA WALIKUA MOJA YA FUKWE HAPA NCHINI
Habari za uhakika zilizopatikana zinasema kuwa binti huyo kwa sasa anahangaika kila kukicha kutafuta ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa Mwijage ili waweze kumshawishi kurudisha uhusiano wao wa mwanzo.

MAPENZI YALIKUA MOTOMOTO KWELI ENZI HIZO
Rafiki wa karibu wa ndugu Mwijage aliweza kutupenyezea habari kuwa majira hayo ya mchana binti huyo alionekana nyumbani kwa Mwijage akilazimisha uhusiano wao kurudia kama zamani lakini ndugu Mwijage alikua na msimamo kuwa hamtaki na hayo mambo kwa sasa yanazungumzwa kifamilia.


NANI ALIJUA KUWA WATAGOMBANA?
Endelea kutembelea blog hii ili tukuhabarishe kitakachoendelea baada ya familia hizi mbili kuzungumza na binti huyu kuendelea kutafuta muafaka wa penzi lake kwa Mwijage.

No comments:

Post a Comment