WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Wednesday, March 6, 2013

BAADA YAKUBUMA JIJINI DAR,MREMBO WA BONGO MOVIE ATIKISA A-city.




Atoa kauli nzito kwa wasanii wa kike “sijachuja,mshikilie uliye nae sichagui kutwa mara tatu”.
Siku chache baada ya kutua katika jiji la Arusha akitokea  jijini Dar mrembo aliyevuma kwa kuharibu ndoa za watu na kutembea na watu maarufu jijini Dar na kufikia hatua yakushindwa kufanya hata sanaa,nakuambulia kuuza sura katika video ya msanii wa muziki jijini aja na jipya jijini Arusha.
Akizungumza na Blog hii msanii huyo aliyefahamika kwa jina la Rose ambaye hivi karibuni aliandikwa na mtandao mwenza na huu baada yakusababisha filamu kushindwa kufanyika akiwagombanisha wasanii waliokuwa wahusika wa filamu hiyo iliyotambulika kwa jina la shadow of pains.
 

Aidha alibainisha kuwa hajachuja hata kidogo na Dar aliondoka baada ya kutamani  kuishi katika mazingira ya baridi kwani alizoea safari za nchi za baridi hivyo bongo kulikuwa kunampa shida na kumuharibu mwili wake uliojazia vema,hata hivyo aliwaonya wasanii wenzake wanaozani amechuja kuwa wawashikilie wanaume zao vema kwani yeye ni zaidi ya kiwembe cha gillete alisema msanii huyo mwenye madoido na jicho la huba.
Licha ya mkwara huo alioingia nao jijini hapa,msanii huyo ambaye anadaiwa kuwa na mahusiano na mtangazaji Jackson John wa kituo maarufu cha radio kinachomilikiwa na mfanyabiashara mkongwe nchini,alijikuta akitulizwa mbwembwe zake na kijana mdogo wa kihaya ambaye ni msanii mwenzake alipokuwa katika mazoezi kwani aliombwa kufanya kipande cha uhusika wa mahaba na kujikuta akihemea juu juu baada ya kuelemewa na ufundi wa chalii huyo mdogo mwenye mambo makubwa na kuzua vicheko kwa wasanii wengine.
Baada ya tukio hilo ndipo minongóno ikaanza kuwa kumbe si lolote si chochote kwani mazoezi yamemnyima pumzi itakuaje katika ukweli,au ndo maana Dar alikuwa anatapatapa nakuachika mara kwa mara,walisikika wenzake wakiulizana.naye hakusita akajibu mapigo kuwa yuko fiti na kuhakikisha hilo atachukua mmoja baada ya mwingine pasipo kujali ni wa nani hata kama mume wa mtu,hata hivyo nyepesi nyepesi nikuwa anataka kuhamia Mwanza kwani Arusha mambo hayalipi kama alivyotarajia.
Kama kawaida ya mtandao huu ,ni kurekebisha tabia hivyo kumuomba dada huyo kutokuaribu tasnia hiyo kwa mkoa huo wala Tanzania kwa ujumla kwani bado mapambano yanaendelea hivyo akafanye kazi nyingine kama sanaa imemshinda…ikumbukwe msanii ni kioo cha jamii na si uhuni.



No comments:

Post a Comment