Baada
ya kuanikwa wazi juu ya kukimbia darasa kwa mrembo mwenye figa matata katika tasnia ya filamu jijini Arusha Mwanahamisi Mziray (Mishi),bidada huyo
amejikuta akizidi kuangukia pua baada ya mambo katika tasnia hiyo kuzidi
kumuendea vibaya na kujikuta akiwapikia wenzake chakula katika kambi waliokuwa
wameweka kabla ya kuanza kupiga kizigo cha filamu yenye utata hadi hivi sasa.
Bishosti
huyo alieonekana kuja kwa kasi katika tasnia hii akiamini ni njia rahisi zaidi
ya kutokea mambo yamezidi kumuendea ndivyo sivyo nakujikuta akitapatapa katika
vikundi.
Chanzo
chetu makini kilitupitishia kavu kavu kuwa bidada Mishi baada ya kuanza vyema
kwa kucheza katika filamu ya Standard 7 alijikuta katika wakati mgumu baada ya
kuibuka kwa shosti mwingine katika kampuni aliyoanza nayo nakufunikwa katika
uchezaji,jambo lililomfanya ahame kampuni nakuanza kusaka vikundi vya sanaa.
Hata
hivyo kama ulivyo msemo wa maisha ni popote,Mishi aliamua kutumia swaga hizo na
kuanza kusaka sanaa kona hadi kona akiambulia kucheza filamu zisizo isha na
kujikuta katika kambi ya kundi la OSG lililokuwa likijianda na kucheza filamu
nayeye kujikuta akipewa kazi yakuwapikia wasanii wenzake hata hivyo alifanya
akiamini atapata nafasi yakucheza filamu.
Aidha
msemo wa kifo cha nyani miti yote kuteleza nao ukadhihilika wazi baada ya bidii
yote ya kuwapikia wenzake akisaka nafasi kutokana na wasanii kuwa wengi,kambi
hiyo ilivunjwa mara kwa mara kutokana na sababu tofautitofauti ikiwemo ngono
nzembe baina ya wasanii nakupelekea kufukuzwa nawahusika wa maeneo waliokuwa
wanaweka kambi.
Baada
ya kashkash hizo,hakuonekana kukata tamaa akijaribu kusikiza msemo wa penYe nia
pana njia lakini mambo hayajaonekana kuwa sawia,hata hivyo blog hii ilizungumza
na baadhi ya wasanii wenzake waliokuwa nae kampuni kipindi cha filamu ya
standard 7 na kumshauri bidada huyo kutokuogopa chalenji hivyo arudi atulie
katika kampuni kwani anazidi kuchuja na kupotea kabisa katika tasnia ya filamu.
No comments:
Post a Comment