WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Friday, March 1, 2013

Msanii azua kashkash kanisa,mchungaji,waumini washikwa bumbuwazi




waumini washika tama wahofu dunia kufikia ukingoni,aibu yamshika msanii atokwa chozi nakujuta.
Mwezi mmoja tu baada ya kanisa la Miracle kufunguliwa na msanii wa kike mjini Arusha aliyeamua kuachana na mambo ya dunia kanisa lake lakumbwa na aibu kama si majaribu toka kwa msanii mwenzake wa zamani aliyeamua kutinga katika kanisa hilo kama mtu aliyeenda katika nyumba ya kawaida kumtembelea rafiki au mtu aendae katika matanuzi kutokana na vazi alilokuwa amevalia.

Ibada ikiwa yaendelea nilipigiwa simu na mmoja wa waumini kuwa katika kanisa kuna jambo la ajabu limejitokeza kwakuwa siko nao mbali fasta nilitoka na kamera yangu mkononi nakwenda kujionea mwenyewe nakupata nyepesi ndipo nilipomkuta binti huyo akiwa kasimama katikati ya kanisa na kumfanya mchungaji kukaa kwa muda baada ya kuona  maajabu ya dunia.

Baada ya muda mzee wa kanisa alionekana akimuomba binti huyo aliyeonekana kutokujali juu ya mavazi aondoke na kwenda kujistiri vema kwani si maadili mema wa nidhamu katika kanisa kwani si sehemu yakihuni,lakini ilionekana kuwa ngumu kwa binti huyo akiamini yuko sawa.

Nao waumini walionekana kuishiwa pozi na wengine walisikika wakisema ama kweli dunia imekwisha kwani huyu binti hana hata chembe ya  aibu?wakati huo mchungaji alionekana kuinama nakuomba na ghafla maombi yakajibiwa baada ya binti huyo kujikuta akitokwa machozi nakuomba kanisa kumsamehe na kumsaidia kwani hakujitambua wala kujua imekuaje alifika katika kanisa wakati alikuwa anaenda katika mambo yake yakawaida.

Baada ya maneno hayo alifunikwa kwa pazia kumsitiri kwani hakukuwa na mwenye kanga na kufanyiwa ibada nakuahidi kuwa muumini mzuri na kuachana na mambo yakidunia.

Msanii huyo  anatamba kwa uchezaji wake wa filamu hivi sasa nakutishia ajira ya mastaa wengi wakike kwa sasa Tanzania.




1 comment:

  1. Hapa ndipo tunapokosea tunapofikiri Kanisani ni mahali pa watu walio watakatifu tuu. Kama ni hivyo Yesu asingekuja na kujichanganya na wenye dhambi. Watumishi wengi na wakristo wengi wamekuwa kama mafarisayo wale ambao walimhukumu Yesu juu ya yule mwanamke kahaba aliyekuwa anamfuta Yesu miguu yake kwa nywele zake na kumpaka mafuta ya thamni au Yesu alipokwenda kula chakula nyumbani kwa Zakayo aliyekuwa mtoza ushuru na akawa amekaa na watoza ushuru mafarisayo wakamtuhumu kwamba anakula na wenye dhambi. Yesu aliwajibu kwamba, wenye afya hawahitaji tabibu na hakuja kwa ajili ya wasio na dhambi bali amekuja kwao wenye dhambi ili waweze kupona.

    Huyo dada Mungu amemleta kwenye madhabahu yake ili apate msaada apone halafu anaonekana kituko badala ya watu wangemhurumia na kumpokea kwa upole na hekima ya Mungu iwasaidie ili wawe msaada kwake apone.

    Marko 16:15-16 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
    Injili ni kwa kila kiumbe. Neno kila maana yake bila ubaguzi kwamba ni kahaba, mlevi, mzinzi, mwizi nk. Sio ajabu huko huko Kanisani kati ya waliokuwa wanamshangaa nao walikuwa wenye dhambi. Sio ajabu walikuwapo waongo, wambeya, wafitini, wanaoenda kwa waganga, wazinzi, wanawake waliokuwa wamevaa mavazi yanayowapasa wanaume, wenye hasira, waliokuwa na uchungu, wanafiki n.k. Lakini ilikuwa rahisi kumnyooshea kidole huyo dada na kumshangaa kwa sababu dhambi yake inaonekana. Bora ya kwake ilionekana ikakemewa. Je ya kwako unayotenda sirini itakemewa na nani kama sio kukupeleka motoni wakati watu wakifikiri uko kwenye safari ya kwenda mbinguni>

    Hivyo namshukuru Mungu kwa ajili ya Mchungaji aliyepata hekima ya kuomba na Mungu akatenda mwujiza huo na ninaamini mbinguni shughuli zote zilisimama kwa ajili ya kumpokea binti huyo. Mungu akubariki Mchungaji. Hakikisheni tu harudi alikotoka, maana kuokoka ni hatua moja na kumfanya asimame na kutorudi alikotoka ni hatua nyingine. Anahitaji msaada pia wa kumwezesha kujitegemea kwa ajili ya vya mwilini. Mungu awabariki sana.

    ReplyDelete