WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Tuesday, March 19, 2013

BAADA YA KIPIGO KITAKATIFU CHA MAGOLI 6 KWENDA RADIO5, KUNDI LA SANAA OSG KUNUSA 5.


 JUMAMOSI HII WABABE WA SOKA KAMPUNI YA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT DIMBANI  TENA.

Baada ya mechi mfululizo za kujiweka fiti kiafya na kudumisha urafiki baina ya makampuni na vikundi vya sanaa jijini Arusha ,kampuni inayokuwa gumzo mjini Arusha kwa kazi safi za filamu pamoja na kusakata kabumbu,jumamosi hii tena kuumana na kundi la sanaa la AYSAG la mjini hapa katika uwanja wa shule ya msingi meru walio na hamu ya kuonja shubiri ya magoli.


Akizungumza na blog hii mkurugenzi wa kampuni babkubwa ya filamu jijini hapa Bw : Elias Magesa ambaye pia ni straika matata afungae dakika za lala salama na kuzua kilio kwa timu pinzani alisema kampuni yake iko fiti kwa mchezo kwani licha ya mazoezi ya sanaa kila siku huanza na mazoezi ya viungo jambo linalowaweka katika ubora kimwili nakuwa tishio katika makampuni na vikundi vya sanaa.
Hata hivyo amewaomba wasanii wa AYSAG kujipanga vema nakufanya mchezo wa kiungwana kwa lengo la umoja wavikundi na sio kuweka mamluki kama walivyo fanya kundi la OSG kwani si lengo la kisanaa na mchezo kwa ujumla,pia aliomba wadada wa kundi hilo kujitokeza kucheza pia ili soka kuwa nzuri na yenye kuvutia kwa lengo la furaha.


Nae mkurugenzi wa kundi la AYSAG Bw: Kim alisema wapo tayari kwa mchezo huo na kuahidi kuweka wadada ili kuwafanya wasanii wote kushiriki vema katika mchezo huo kwani hakutakuwa na mchezo wa pete nakuahidi mchezo wakiungwana na furaha akisema wanajua maana ya michezo na sanaa.

Nae Kapteni wa timu ya Kampuni ya Emags Ibrahim Jamal amewaomba wasanii wote kuwahi uwanjani ili kuanza mapema na kuhitimisha kwa furaha za kisanaa,akitoa angalizo la AYSAG kuwa makini kwani wataondoka na kapu la mabao na kuomba wadau kujitokeza kushuhudia kandanda safi.
Aidha blog hii inawatakia mchezo mwema na wenye furan a amani na pia kuahidi kuwapa wasomaji matokeo kila baada ya dakika ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment