WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Tuesday, March 12, 2013

MUIGIZAJI WA KIUME ADAIWA KUMTESA MPENZI WAKE : NI BINTI ALIYEANZISHA KANISA LA MIRACLE


 Mcheza filamu na mwandishi wa habari jijini Arusha anayesifika kwa kupenda mauzo atambulikae kwa jina la Deogratius anadaiwa kumtesa mpenzi wake kimapenzi na kumsababishia  baadhi ya makovu mwilini akijiumiza kwa kusudi kwa imani ya kupunguza hasira.


Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa bidada huyo ambaye ni mchungaji wa kanisa la Miracle alilofungua baada ya kutemana na mzigo wa kuuza sura yaani muigizaji (jina kapuni),alidai kuwa shosti huyo kwa sasa anashindwa hata kufanya shughuli nyingine kisa kulilia penzi la HB huyo ambaye amekua kama Jaguar na nyimbo ya kigeugeu.



“mimi namshangaa sana rafiki yangu huyu,ni mwaka na miezi hivi sasa anamngángánia huyu jamaa sijui karogwa?sasa alisema kaacha mambo ya dunia nakuanzisha hadi kanisa ndugu mwandishi wewe ni shahidi ulikuwepo kipindi kanisa laanzishwa,mimi nimemshauri sana basi hata atafute mume lakini hasikii,kafa kaoza kwa huyu jamaa kweli nimewahi kupenda lakini huyu rafiki yangu kazidi’’alinukuliwa akisema binti huyo.

Hata hivyo nyepesi za chini chini zinadai hali ya shosti huyo kuwa mbaya kwani kuna wakati anaonekana kuvimba macho kama mpiganaji masumbwi kwakushinda ndani akilia kama mtoto mdogo jambo linalo mkra swaiba wake huyo.

Aidha Blog hii ilimtafuta Deo na kuzungumzia ishu hii,hivi ndivyo alivyotiririka, “kaka hayo majungu tu,mimi nampenda sana mpenzi wangu,kwanza wamzungumzia yupi?


Haaaaaaaaaa akajikuta anajishtukia kwani hakujua anayezungumziwa ni yupi kwa wakati huo,nikabaki najiuliza anawangapi?lakini nikampa ufafanuzi akatiririka.

“aha kumbe huyo,kaka mi nampenda sana mpenzi wangu na hivi tunavyozungumza mwezi wa nane namaliza mambo,nafunga nae ndoa we jiandae kula pilau tu”.

Baada ya mazungumzo hayo bidada muolewaji naye alitafutwa na kuulizwa kama alikuwa na taarifa juu ya ndoa hiyo ya mwezi nane, “mh ndoa ya nani tena ndugu yangu mana mi nikama nagundu mahusiano yakawaida yananipa kichefuchefu hiyo ndoa ya wapi labda 2015 nikijaaliwa”.heeeeeee kumbe hata hakuna cha ndoa.

Hata hivyo jamaa huyo ameombwa kuwa muangalifu kwani anamfanya binti huyo kuwa mlevi sana kwa sasa jambo linalowaogopesha wasanii wengine kuwa atakuja kunywa hata sumu.

No comments:

Post a Comment