WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Tuesday, March 12, 2013

MWAMUZI MBELEKO KWA KIKUNDI CHA SANAA OSG,EMAGS KAMA ULAYA KABAAAANG!



KIKOSI CHA MAUAJI CHA EMAGS

Wasanii wa filamu kutoka kampuni ya Emags Video Entertainments mwishoni mwa wiki waliwafundisha mamluki wa kikundi cha OSG  soka la kiulaya na kuwaacha mashabiki wakinongóna wakiifananisha timu hiyo na timu za ligi kuu bara, na zile za ulaya kwa kiwango walicho kionesha.

IBRAHIM JAMAL AKIINGIA UWANJANI

RODGERS AKIWAITA WACHEZAJI KUFANYA WARM UP

Mechi hiyo iliyokuwa imejaa kila aina ya mbwembwe za kisanii na majigambo toka kwa viongozi na mashabiki wa timu hizo hususani mabinti waliokuwa wamefulika katika kiwanja cha shule ya msingi meru,kilishuhudia kipute hicho kikikamilika kwa pacha ya goli nne kwa nne licha ya kucheza dakika  zaidi ya tisini kwa utashi wa refa aliokuwa akiwatafutia goli OSG waliokuwa nyuma kwa mabao 4 kwa 3 hadi dakika tisini.

Kuonyesha kuegemea upande mmoja mwamuzi wa mchezo huo aligomea goli la tano la Emags baada ya shuti kali lililopigwa na kiungo mchezeshaji wa emags Mau na kumshinda kipa wa OSG na refa kulikataa akidai hakuwa ameruhusu mpira kuanza.

Naye mkurugenzi wa OSG bwana Isack aliyejigamba kushinda mechi hiyo kutokana na kuwa na mamluki wanaocheza ligi ya wilaya Arusha alijikuta akikaa chini baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo,kwani angewalipa fedha mamluki hao pasipokuwa na ushindi.

Aidha upepo ulizidi kuwa mbaya kwao kwani walijikuta wasanii wao wakihamia upande wa Emags na kuanza kuwashabikia mastaa wa filamu toka kampuni hiyo ya Emags  na hata kuomba kupiga nao picha baada ya mchezo jambo ambalo lilimkera bwana Isack na kugomea michezo siku nyingine akidai kuwe na semina za sanaa si michezo kwani haina faida kwao kama kuigiza.

Hata hivyo kila penye wengi hakukosi jambo kwani baada ya mchezo vijana hao waliokuwa wamekodiwa walijikuta wakilipwa pesa chini ya makubaliano nakujikuta wasanii wa osg wakichangishwa tena ili kuondoa aibu ambayo ingetokea mbele ya kadamnasi iliyokuwepo jambo ambalo lilishuhudiwa na paparazzi wa blog hii.

Magoli ya Emags yalifungwa na Maulidi (Mau) -2, Arnold(Dizo),-1  pamoja na kijana mrefu na machachari Aloyce aliyefunga 1 pia,kwa upande wa OSG majina ya wafungaji yalishindikana kupatikana kwania hata mkurugenzi wao hakuwajua majina.

Aidha mchezo ulimalizika bila ugomvi na kufungwa na mkurugenzi wa kampuni ya Emags Bw: Eliasi Magesa aliyetishia amani ya mabeki wa OSG kwa kuwalamba chenga sana na kupiga mashuti makali yaliompa kipa wakati mgumu licha ya umri kuwa mkubwa.naye aliitimisha kwa kuomba michezo iendelezwe ili kuleta urafiki mzuri na pia wasanii kufahamiana ,lakini akiwaomba timu za makampuni ya uma na binafsi ,pamoja na wasanii wa Bongo movie kujipima kwa timu ya Emags kwani iko vema .

Emags ilianza vema kushiriki michezo ilipoitililishia mvua za magoli timu ya Kings Entertainment ya mzee majuto mjini Tanga magoli 9 kwa 2,radio 5 Arusha waliopata kipigo cha bao 6 kwa 1 na OSG waliolazimisha sare kwa kucheza dakika 130 ili kusawazisha

PICHA ZA MATUKIO YA UWANJANI

CAMERAMAN DENNIS ALIKUA AKIFANYA YAKE

BENCHI LA EMAGS WAKIWA WANASHANGILIA

BENCHI LA UFUNDI LA OSG


DIZZLE MAN DILLUNGA AKIPIGA PENALTI

DEO G "GOALKEEPER WA EMAGS"

BENCHI LA EMAGS WAKATI WA MAPUMZIKO

BENCHI LA EMAGS WAKATI WA MAPUMZIKO

EMAGS WAKIFANYA WARM UP KABLA YA MECHI

MAPUMZIKO WACHEZAJI WAKIBADILISHANA MAWAZO

RODGERS, DIZZLE NA MAURICE WAKISHANGILIA GOLI

HEKA HEKA GOLINI MWA OSG

WACHEZAJI WAKIRUDI UWANJANI KUCHEZA KIPINDI CHA PILI

HEKA HEKA ZA UWANJANI

OSG WAKIFANYA WARM UP KABLA YA MECHI

IBRAHIM JAMAL AKIMPA GOALKEEPER DEO G MAZOEZI KABLA YA MECHI

No comments:

Post a Comment