WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Friday, March 1, 2013

ARUSHA PROFESSIONAL YATIBUA MAMBO,YAWA MWIBA MCHUNGU KESI ZATAWALA OFISINI KWAO



Ikiwa  ni siju chache tu baada ya mtandao wa kurekebisha tabia na kutangaza sanaa ya jijini Arusha kuanzishwa hali zimekuwa tofauti kwa wasanii mjini hapa baada ya baadhi kuonekana kufurahia hali hiyo huku wengine wakionekana kuchukizwa na. kujawa jazba mara kwa mara baada ya kamera ya blog hii kuwanasa katika matukio na kuandikwa .
Katika matukio makuu mawili ya hivi karibuni yalioandikwa juu ya msanii wa ngoma asili na ile ya msanii wa kike kuwatia tumbo joto wenzake kwa kutembea na mabwana zao  kutapakaa walionekana kutoridhika baada ya kukumbwa na simu zisizoisha juu ya matukio yao kutoka kwa watu wanao wafahamu na kuhofu mambo yao kubuma.
Wasanii hao kwa nyakati tofauti walifika katika ofisi za blog hii na kuripoti juu ya maumivu wanayopata kwani hawakujua mambo yangekuwa kama yalivyo baada yakuandikwa katika mtandao,vurugu za hapa na pale zilijitokeza lakini kupitia kwa mwanasheria wa Blog hii Severinus Mwijage mambo yalikaa vema kwani hawakuwa na lakujitetea baada ya kusomewa vipengele vya sheria ya blog na taratibu za habari kwani story ikiwa balanced ni haki kuwekwa hadharani.
hata hivyo baada ya siku kadhaa walirudi nakuishukuru  blog hii kwani imewasaidia kuachana na mambo mabaya nakujikita katika kufanya sanaa kwa uadilifu mkubwa na hata kuwa makini katika kila jambo kwa hofu ya kuandikwa tena katika mtandao.
Safu ya wahariri inawaomba wasanii kuwa huru kufikisha habari zao zenye maendeleo na si kufanya mambo ya skendo nakulalamika wanapoandikwa,aidha iwewasii wasanii wavikundi vyote kutoa kazi nyingi nakuzitangaza kupitia mtandao huu bila ya gharama yeyote.

No comments:

Post a Comment