WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Tuesday, February 26, 2013

WASANII WA FILAMU WAJITOSA SHINDANO LA THE YOUNG MILLIONAIRE REALITY TV SHOW KUWANIA TSH 10,000,000




Lile shindano la kumtafuta kijana mwenye kipaji cha ujasiriamali linaloendeshwa na kampuni mahiri ya kutengeneza filamu, documentary na upigaji picha wa aina zote za video ya Emags Video Entertainment iliyopo Jijini  Arusha litakaloanza kurushwa hivi karibuni kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1) limeingiliwa.

Habari za uhakika toka kampuni ya Emags Video Entertainment zinasema kuwa shindano hilo litaanza kurushwa hivi karibuni na washiriki wanaendelea kujisajili kwa wale wa mkoa wa Arusha tu.
Katika kuonesha vipaji vyao vya ujasiriamali, wasanii pia nao wameamua kuingia katika kinyang’anyiro hicho cha kugombea shilingi 10,000,000 (milioni kumi za kitanzania). Wasanii hao waliochukua fomu ni pamoja na 

Mwanahamisi Mziray a.k.a Mishy
Fred Kadege
Charles Mwise
Abby Carter na
Lilian Urassa
Pia akizungumza na mwandishi wetu Afisa Uhusiano wa kampuni ya Emags Video Entertainment ndugu Severinus Mwijage Jr amesema “Kwa sasa tuna mshukuru Mungu tumemaliza usahili katika mikoa mbalimbali kama Mwanza, Kagera, Morogoro, Dodoma, Musoma, Kilimanjaro, Tanga na Manyara”

Aliongeza pia “Mkoa wa Arusha ndio tunafanya mchakato wa kupata washiriki, kwa wale wanaotaka kushiriki shindano hili wafike katika ofisi zetu zilizopo tank la maji Ilboru Jijini Arusha kwani nafasi zipo chache”

Afisa Uhusiano huyo aliendelea kusema kuwa “ Ndugu mwandishi tunavyozungumza sasa tumetoka katika hoteli ya PENGUIN RESORT HOTEL iliyopo Sakina Jijini Arusha na tumezungumza na Meneja wao na wametoa ruhusa ya shindano hili kufanyika katika hoteli yao, tunawashukuru sana uongozi wa PENGUIN RESORT HOTEL kwa kukubali kuinua vipaji vya vijana katika Nyanja ya ujasiriamali”
Blog hii inawatakia kila la kheri wasanii hao ili waweze kufikia malengo yao.

Kwa wale wanaotaka kushiriki shindano hili la THE YOUNG MILLIONAIRE REALITY TV SHOW wenye umri kati ya miaka 18 hadi 30 unaweza kuwasiliana na Emags Video Entertainment kupitia namba zifuatazo

+255 754 014 227                                    
+255 656 396 025


No comments:

Post a Comment