Lile
shirikisho la filamu Jijini Arusha ambalo linasemekana liliundwa kiujanja
ujanja na kupewa jina la ARUSHA MOVIE kwa sasa hakukaliki na hii ni baada ya
tetesi zilizotufikia kuwa wanachama wa shirikisho hilo ambao pia ni viongozi
wameanza kulogana.
Hayo
yamebainishwa na mtoa taarifa wetu baada ya Katibu Mkuu wa shirikisho hilo la
filamu Arusha (ARUSHA MOVIE) ndugu ISAACK ambaye pia ni mkurugenzi wa kikundi
cha sanaa cha OSG, kulazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru huku akiwa
amewekewa drip tisa ndani ya muda mchache na kwa majibu ya Daktari ni kwamba
ugonjwa haukuonekana walipo mfanyia vipimo kwa mara ya kwanza.
Hata
hivyo baadhi ya wasanii ambao ni wanachama wa ARUSHA MOVIE walipoulizwa juu ya
sakata hilia walisema kuwa “Ni kweli mambo haya yapo ya kulogana kwani kumezuka
hali ya sintofahamu kwa viongozi wetu huku wengine wakizushiana skendo, kiongozi
mmoja jina kapuni inasemekana alifumaniwa na mke wa mtu”
Kwa
upande wake ndugu ISAACK alipotafutwa kuzungumzia sakata hili yeye alisema kuwa
“Ni kweli ndugu mwandishi nililazwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa
siku kadhaa na pia nilitundikiwa dripu takribani tisa, hiyo ni kutokana na
kukutwa na ugonjwa wa malaria baada ya madaktari kuchukua vipimo kwa mara ya
pili”
www.arushaprofessionalmovies.blogspot.com itaendelea
kufuatilia sakata hili la ARUSHA MOVIE na kuwaletea habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment