WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Wednesday, February 13, 2013

MSANII WA FILAMU AAMUA KUFUNGUA KANISA LAKE KISA…………………

POKEA  UPAKO MTAKATIFU
 Lile wimbi la kuongezeka kwa makanisa nchini Tanzania linaloongozwa na mikoa ya Mbeya na Arusha kila kukicha linaendela kushika kasi katika Jiji la Arusha baada ya msanii wa filamu ambaye pia ni mfanyakazi katika hoteli moja maarufu hapa jijini Arusha kuamua kuanzisha kanisa lake mwenyewe.

Hayo yalibainika pale mtoa taarifa hii alipotuambia kuwa msanii huyo kwa sasa baada ya kuona anateseka kimapenzi kwani kila kukicha wanakorofishana na mpenzi wake hivyo kuamua kumrudia Mungu na kufungua kanisa lake.

Kwa habari za uhakika kutoka maktaba yetu  inasema kuwa binti huyu kila kukicha anaonekana akiwa na mawazo na pia muda mwingi huwa anaonekana hana raha hasa pale anapomkumbuka mpenzi wake huyo ambaye jina tunalo na wanaomfariji mara nyingi ni marafiki zake wa kiume.

Hizi ni picha ambazo mtoa  habari wetu alitutumia alipokwenda kusali katika kanisa hilo na kusema kuwa kwa kweli huyu dada ana UPAKO kupitiliza…

ANAYESADIKIKA KUWA MCHUNGAJI WA KANISA JIPYA LA DELIVERENCE MIRACLE CENTER
Kanisa la huyu dada liko maeneo ya Ilboru na linaitwa DELIVERENCE MIRACLE CENTER mita chache toka barabara kuu ya Moshi – Arusha na kwa ratiba ya Ibada ni kama ifuatavyo:-

Jumatatu – Maombezi    -  11:00 jioni – 12:30 jioni
Jumanne – Neno   -  11:00 jioni – 12:30 jioni
Jumatano – Ibada ya kusifu na kuabudu  -  11:00 jioni – 12:30 jioni
Alhamisi – Maombi na Maombezi      - 11:00 jioni – 12:30 jioni 
Ijumaa – Maombi ya kufunga              -   11:00 jioni – 12:30 jioni
Jumamosi – Kwaya                     -        11:00 jioni – 12:30 jioni
Jumapili – Ibada ya Neno la Mungu                    -     4:00 asubuhi – 8:00 mchana
                             Maombezi     -  11:00 jioni – 12:30 jioni

No comments:

Post a Comment