Baada
ya kashfa nzito ya ushirikina ndani ya
wasanii wa Arusha movie,kwa kile
kilichodaiwa katika toleo la mwanzo la mtandao huu kurogwa kwa katibu wa klabu
hiyo Bw.Isack ambaye pia ni mkurugenzi wa kikundi cha sanaa OSG jijini hapa
,katibu huyo amejitokeza hadharani na kuweka mambo wazi huku akidai kupona kwa
dripu 9 za kwinini.
Hata
hivyo akionesha kuwa fiti nakuanza majukumu yake kama katibu,alionekana katika
kituo cha polisi mjini kati akiwa na jazba na kumburuza mwandishi wa mswada wa filamu walio tarajia kuicheza
ijulikanayo kwa jina la “the bodyguard
of Queen”.
Mshtakiwa
huyo aliyefahamika kwa jina la Charity Klavery alidaiwa kuwaraghai wasanii wa kundi la OSG na wengine waliojitokeza
kucheza filamu hiyo,huku akidai kuwa amepata ufadhiri kutoka kwa mwanamuziki maarufu wa injili
kutoka nchini Kenya “jina
tunalihifadhi”,na kuwafanyisha mazoezi kwa muda mrefu bila ya malipo akiwemo
mjane wa mwanamuziki maarufu aliyewahi kutamba jijini Arusha na Afrika
Mashariki kwa ujumla kwa nyimbo za kuabudu.
Hata
hivyo mjane huyo alishtukia janja ya nyani ya Bw.Charity nakuamua kuachana nao
baada ya kushindwa makubaliano ya malipo ya kucheza filamu hiyo kwani alipaswa
kucheza kama muhusika mkuu yani Malkia.
Mambo
hayakukaa vema kwani Charity alishindwa hata kuleta mswada huo na kuamua kuleta
muongozaji wa filamu mwingine kutoka
mjini Moshi aliyetambulika kwa jina la Ibra aliye wahi kusimamia filamu za
msanii maarufu nchini kwa jina Ray ,ambaye aliwakataa wasanii waliokuwepo
nakutaka wasanii wapya jambo lililosababisha mvutano kati yake na katibu Isack
aliyekuwa msimamizi wa awali.
Aidha
baada ya vuta ni kuvute hiyo,Isack aliamua kutumia nguvu za dora kupata haki za
wasanii wake ,ndipo aliamua kumburuza Charity kituo cha polisi nakudai fidia
kwa kupotezewa muda jambo lililokuwa gumu kwa upande wa Charity nakuamua kuwapa
muswada wa filamu hiyo kama fidia jambo lililotekelezwa mbele ya mwanasheria .
Hata
hivyo licha ya kupewa muswada huo haijajulikana filamu hiyo itachezwa lini
kwani hali ya uchumi bado ni tete.
No comments:
Post a Comment