WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Saturday, February 23, 2013

MSANII ANAYEWALIZA WENZAKE AFUNGUKA KISA


MAUREEN / HAPPY

Baada ya habari juu ya kuwaliza wenzake kutapakaa ,msanii Maureen alizama moja kwa moja katika ofisi za blog ya Arusha professional nakudai kuwa hajawaliza wenzake wala si kweli kuwa anatembea na big boss huyo wa utalii.

Akizungumza kwa jazba na mwandishi wetu, “kwanza ndugu yangu nikwambie hao wanaosema juu yangu nikuwa wanataka kusafiria nyota yangu hata sijatoka maskini,lakini mi nikuweke plain tu kuwa sina mahusiano zaidi ya kuwa na urafiki tu wa kawaida na huyo kaka,mimi nina mchumba wangu ambaye yuko Ufaransa hivyo hao lengo lao nikutaka kuniharibia tu.

Baada ya maelezo hayo akafunguka juu ya ugomvi wake na msanii mwenzake anayetembea na pedeshee huyo akatililika “sina ugomvi na mtu wala sina mda wakushea na mtu,kama yeye anasema nimemuingilia basi nimemuachia aendelee nae mi nina mambo yangu na sina muda wakupoteza”.

Haikuishia hapo ,ghafla akaanza bonge ya vurugu na mwandishi wa habari ya blog hii, “mi sitaki kuandikwa kwanini mnifuatilie?mnajua nina tegemea ndugu zangu unazani wakiona nitawajibu kitu gani ,mi nawaheshimu naomba na nyie mniheshimu”alinukuliwa akisema Maureen.

Aidha haikupita masaa kabla ya kutoka katika ofisi zetu akabambwa tena akiteta na wasanii wenzake kuwa hivi karibuni lazima awe star kupitia mtandao huu na kuwa alikuwa anazuga tu kugombana na mwandishi ila ni ishu sana kuandikwa.

Hata hivyo blog hii haitasita kukuletea lolote litakaloendelea katika baragumu hili la mastaa watarajiwa wa bongo movie lakini tukiwahasa kutoendelea na tabia za bifu na mambo ya kashfa bali wazingatie sanaa  ili kuelimisha jamii kwani kashfa si dilii nomaaaa….

No comments:

Post a Comment