WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Friday, February 22, 2013

MUUZA SURA WA KIKE AUMBUKA MSIBANI



Ashindwa kujifunga khanga,azitupia nakutia wenzake aibu…
MSANII WA FILAMU ALIVYOFUNGA KANGHA MSIBANI KAMA ANAENDA BAFUNI
 Msanii mwenye sura ya mauzo mnamo tasnia ya filamu  jijini Arusha aliyefahamika kwa jina moja la Jack almaarufu kama Baby Face,amejikuta akiingiwa aibu ya mwaka alipoburuzwa na wenzake kwenda kuhudhuria msiba wa mmoja wa wasanii wenzake aliyefiwa na baba yake mzazi katika maeneo ya Sakina kitaa cha Silent Inn.

JACKY KATIKA POZI MSIBANI
 Bishosti huyo alikubwa na balaa hilo pale alipokaribia maeneo ya msiba na kutoa khanga zake kwaajili yakujistili nakutia fola baada ya kushindwa kujifunga na khanga kumuanguka chini kila aliposogeza hatua moja,jambo lililowafanya wenzake kusimama kwa dakika kadhaa wakimsaidia namna ya kujifunga ili waingie eneo la msiba.

JACKY MAUZO
 Aidha licha ya kusaidiwa alionekana kutokuwa mzoefu wa mitoko hiyo na kujifunga kama mtu aendae bafuni akiacha kichwa wazi kilichokuwa na staili iliyowafanya waombolezaji kumkodolea macho kwa muda mrefu wakimfananisha na msanii nguli Jackline wolper huku wengine wakinong’ona kuwa ni mdogo wa Amber Rose huyo wa bongo.

AKIONEKANA MWENYE FURAHA MSIBANI BADALA YA HUZUNI
 Kuonesha kutokujali msanii huyo alitupia headphones zake katika masikio na kuendelea kula ngoma za kibongo nakujisahau kuwa alikuwa katika eneo la msiba na kuwafanya wenzake kuinamisha vichwa kwa muda kukwepa aibu hiyo.

AKITAFAKARI NAMNA YA KUFUNGA KANGHA
 Hata hivyo Arusha professional inamuomba kisura huyo kubadili mapigo nakujichanganya katika mazingira yote kwani yeye ni kioo cha jamii na kuwaomba wasanii wengine kutofautisha maisha yao yakisanaa na kisupastaa hata katika mambo yasiyofaa.

No comments:

Post a Comment