WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Thursday, February 21, 2013

BAADA YA KUTESEKA MUDA MREFU KUZIMU NA KUFUNGULIWA AAMUA KUINGIA KWENYE SANAA

 


Kisura mdogo anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka kati ya 18-19,(jina tunalihifadhi)aliyekuwa amechukuliwa msukule kwa takribani miaka nane iliyopita ,amejitokeza hadharani na kujikita moja kwa moja katika tasnia ya filamu za bongo.

Binti huyo mwenye kila sifa yakuitwa mrembo,aliyewahi kushiriki mashindano ya ulimbwende katika shindano la miss Arusha,akiwakilisha kitongoji cha Sakina na kuwatoa jasho warembo wengine zaidi ya 20,alinaswa na kamera za Arusha professional movies akiwa bize katika kikundi kimoja cha sanaa kinachokuja kwa kasi mjini hapa kinachodaiwa kumilikiwa na diwani wa chama cha upinzani jijini Arusha.
Akihojiwa na mwandishi juu ya ujio wake huo,binti huyo alionekana kujigamba kuwa ameingia katika tasnia hii kwa lengo la kufanya mapinduzi licha ya changamoto za kusumbuliwa na majibwana na hata wasanii wenzake kumlazimisha kula nae chakula chakiutu uzima jambo linalo mpa wakati mgumu wakufikilia mapinduzi yakisanaa lakini akiahidi kupambana nawakware hao.


“nikweli nilikuwa katika dunia nyingine japo si kwa kukusudia,nimefanya mengi ikiwemo kula nyama za watu,kusababisha ajali,na hata kuua pasipokujitambua,lakini namshukuru Mungu na askofu wangu aitwae Macha kwa maombi hadi kuwa hivi nilivyo sasa,kweli namshuru sana Mungu kwani sasa ntatimiza ndoto yangu yakuwa msanii bora wakike Tanzania na Dunia kwa ujumla”

Aidha aliwaomba wasanii wenzake kutokujali juu ya matukio yake ya awali kwani hakujua kilichotokea nakuomba ushirikiano hili kusongesha gurudumu la sanaa Arusha na Tanzania kwa ujumla.
Hata hivyo aliwaonya wasanii na wadau kutokumsumbua katika ishu za mapenzi kwani hakuingia katika sanaa kwa lengo la kujiuza bali kufanya sanaa kama kazi.


 

No comments:

Post a Comment