WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Friday, February 22, 2013

HII INA KUHUSU




EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT YASAKA VIPAJI VIPYA VYA WAIGIZAJI. 



Kampuni maarufu ya utengenezaji wa filamu jijini Arusha,ambayo imejizolea umaarufu mkubwa baada ya kutoa filamu kadhaa ikiwemo “Mateka wa kiroho,Standard 7,tamthiliya ya Haiba ya penzi na kutengeneza kazi nyingine kibao ikiwemo Nampenda motika,Chozi la yatima na mzigo unaotarajia kudondoshwa sokoni na wasambazaji namba moja Steps uliobeba jina la Temptation of my wife lakini pia wakitarajiwa kuwa na reality show kali inayokuja hivi karibuni kupitia Tbc1 iitwayo “young millionea”.

DIRECTOR WA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT AKIWA KAZINI
 Akizungumza na Blog hii,mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw:Elias Magesa amesema kuwa “lengo la kampuni ya Emags nikukuza sanaa ya Tanzania,na tunamshukuru Mungu tumeweza kufanikiwa kufanya kazi nyingi kama nilivyokuainishia ndungu mwandishi”.

DIRECTOR WA EMAGS NA WASANII WAKIWA LOCATION
Akiendelea kuzungumza na mwandishi wetu Bw.Elias Magesa aliendelea kusema kuwa kwa sasa wametoa nafasi kwa vijana na watu wazima kuonesha vipaji vyao vya kuigiza kwani kwa sasa wanaandaa tamthiliya itakayorushwa na televisheni maarufu hapa nchini,na pia kuendeleza wimbi la kutoa filamu kwani kwa kuanza wanataka kupiga filamu mpya ya Lost Orphans,hivyo wahi nafasi kwani waweza kuwa kinara.

WASANII WA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT WAKIFANYA YAO
Aidha alitoa namba za simu kwa yeyote atakae kuwa tayari kujiunga na kampuni kuwa ni 0754-014227/0656-396025/0787-661199 na 0658-288054.

MAMBO YA LOCATION HAYA

DIRECTOR WA EMAGS AKIFANYA MAMBO YAKE

MOJA YA CAMERA ZINAZOTUMIKA NA KAMPUNI YA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT

HAPA KAZI TUUUUUUUUUU

HAKUNA KUCHEKA KAZI TUUUUUUUUUUUUUU

No comments:

Post a Comment