WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Thursday, February 7, 2013

MSANII WA FILAMU NA NGOMA JIJINI ARUSHA AKANA KUMPA BINTI MWENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 UJAUZITO




MASS B KAZINI
 Msanii wa sanaa ya maigizo na ngoma kutoka kundi maarufu la AGESTA anayekuja kwa kasi toka jijini Arusha  na kutambulika kwa jina moja la Silivia,amejikuta akizima ndoto zake za sanaa  katika umri mdogo pamoja na ajira yake katika shirika moja la kutetea haki za watoto lililoko mjini hapa pasipo kutarajia huku akiwaacha midomo wazi  wasanii wenzake kwa tukio lililomkuta hivi karibuni.

Bishosti huyo anayekadiriwa kuwa na umri chini ya miaka 18 amejikuta katika aibu yakufunga mwaka 2012 na kufungua mwaka huu wa 2013 kwa aibu ya namna yake  baada ya kupewa mimba au kwa lugha nyepesi  “kuwekewa kitumbua chake mchanga” na msanii mwenza wa kundi hilo ajulikanae kama Masanja almaarufu “ Mass B”.
Hata hivyo balaa lilizidi kumkumba bidada huyo kwani alijikuta akilea mimba hiyo pasipo msaada wa Mass B aliyekuwa amekana kuhusika kwa ishu hiyo kwani anaye mchumba  anaye ishi jijini Mwanza na alikuwa katika mipango ya ndoa.
Aidha baada ya muda baadhi ya wasanii wakaribu na Mass B walitumia sanaa kumshawishi kijana huyo,na mwisho wa siku kujitia kitanzi na kukiri kuwa muhusika wa zigo hilo na kutoa huduma zote kwa binti huyo mdogo.
Haikuishia hapo kwani jamaa aliomba ridhaa ya kuishi na Silivia kwa lengo la kutoa malezi ya mimba ,naye mlezi wa binti huyo hakusita aliwapa  ruksa na sasa wanaishi pamoja mitaa ya Sakina.
Hata hivyo mtandao huu unampongeza binti huyo kwa kujifungua salama mtoto wa kike,nakuomba wasanii kuwa makini na kutimiza ndoto zao kwa faida ya sanaa ya Tanzania.

MASS B NA SILVIA


No comments:

Post a Comment