WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Thursday, February 21, 2013

MSANII WA FILAMU ARUSHA AJITAMBUI KUWA YEYE YUKO KUNDI GANI LA WASANII TANZANIA

XAVERY MAZUKE a.k.a AMX
 Msemo  wa usilolijua ni sawa na usiku wa giza umedhihilika kwa mshangao mkubwa katika tasnia ya sanaa Jijini Arusha baada ya msanii mmoja kutoa kali ya mwaka katika kituo cha redio maarufu mjini hapa ndani ya kipindi cha Mtaa wa pili .


Msanii huyo aliyevuma na filamu ya kimasai iliyotamba kwa jina la Nampenda Motika,anayefahamika kwa jina la XAVERY MAZUKE a.k.a AMX,ambaye alipigiwa simu pasipokujua na mwendesha kipindi wa redio hiyo na kuulizwa juu ya kazi zake,na ghafla kuulizwa juu ya sanaa ya mkoa huu ,alijikuta akionesha umaarufu kabla hata ya kufikia kiwango hicho nakujikuta akijichanganya kwa jambo asilolijua huku akiongea kwa kujihami kama mtu anayejua .


Baada ya mjadala wa muda ndipo aliulizwa kutambua juu ya shirikisho la filamu jijini hapa ujulikanao kama Arusha Movie pamoja na mtandao wa kijamii uzungumziao mambo ya burudani na sanaa kwa ujumla wa Arusha professional movie,na akatililika bila woga.


Akinukuliwa “ah kwanza mi sitambui juu ya Arusha movie zaidi ya kusikiasikia tu maana si wa levo yangu na siwezi kuwa katika shirikisho lililo na migogoro na viongozi wasio wa umoja kama jina lilivyo”na kisha akaulizwa kama anatambua Arusha professional  “ha ha ha (kicheko kwanza) ebana unajua hawa jamaa wanataka kuiga Dar wanavyogawana bongo movie na bongo unity pasipokujua maana halisi ya majina hayo,sasa hawa Arusha Professional wameibuka baada ya kuona arusha movie sasa mi sijui shirikisho lipi sahihi ila natamka wazi kuwa sitambui makundi hayo mawili kwani hayko kihalali”mwisho wa kumnukuu.


Baada ya maelezo yake alipigiwa simu na Arusha professional nakufafanuliwa kuwa huu ni mtandao wa kijamii wa kukuza sanaa kupitia habari zao na kazi zao na si shirikisho kama alivyodai katika kituo cha redio,hapa jijini naye aliomba radhi kwa kuchanganya mambo kwani alipigiwa simu ghafla sana na hakuwa amejipanga  .


Aidha www.arushaprofessionalmovies.blogspot.com inatoa rai kwa wasanii na jamii kwa ujumla kutoihusisha mtandao huu na mashirikisho au kampuni ya mtu yeyote kwani ni mtandao wakijamii.

No comments:

Post a Comment