|
WAIGIZAJI WA FILAMU TOKA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATOTO WA KITUO CHA FARAJA ORPHANS CHILDREN HOME |
Kwa
kawaida siku ya wapendanao duniani huadhimishwa kila tarehe 14 mwezi February kila
mwaka na siku hii ni maalumu kwaajili ya
watu wote wenye upendo.
Mara
nyingi watu wengi wamekua wakiiadhimisha siku hii kwa kuwa karibu na wapenzi
wao na wake zao na kusahau kuwa siku hii huwa ni maalumu kwaajili ya watu wote
kama ndugu, jamaa na marafiki na zaidi ya yote kwenda kuwaona wenye shida
mbalimbali kama wagonjwa, walemavu , wajane na yatima.
Kwa
kuonesha kuwa siku hiyo ni maalumu kwaajili ya watu wote na sio wapenzi tu, waigizaji
toka kampuni ya EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT waliweza kuonesha upendo wao kwa
kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha FARAJA ORPHANS CHILDREN HOME
kilichopo Jijini Arusha eneo la SHANGARAI wilayani ARUMERU.
Waigizaji
hao walipoenda kituoni hapo waliwapelekea watoto hao vitu mbalimbali kama
madaftari, penseli, sabuni, vyakula,sukari
na vitu vingine mbalimbali na baadaye wakaenda kucheza mpira wa migumuu
na watoto wa kituoni hapo kuonesha kuwa wanawapenda sana.
Watoto
hao walifurahi sana kutembelewa na waigizaji hao wa kampuni ya EMAGS VIDEO
ENTERTAINMENT na kuomba kutembelewa tena siku za usoni na sio siku ya
wapendanao tu bali wakati wowote wanakaribishwa.
|
BWANA FARAJA - MLEZI WA FARAJA ORPHANAGE CHILDREN HOME |
Hata
hivyo Mlezi wa kituo hicho Bwana Faraja aliweza kuelezea historia ya kituo hicho kwa kuanza kusema “Mimi
niliamua kuanzisha kituo hiki kutokana na vipimo vya kitaalumu kuonesha kuwa
mimi sina uwezo wa kupata mtoto yaani siwezi kuzaa, nikaamua kuadopt (kuasili) watoto watatu, lakini baadaye wakapata
ufadhili wakaenda kusoma nje ya nchi”
Bwana
faraja aliendelea kusema kuwa “ baadaye pia niliweza kuadopt (kuasili) watoto
wengine watatu, ndipo nilipopata ushauri kutoka serikalini kwamba kuna leo na
kesho hivyo ni vyema nifungue kituo cha watoto yatima na kuweza kukisajili ili
kijulikane kisheria”
Hizi
ni baadhi za picha na matukio mbalimbali yaliyofanywa na waigizaji hao wa
kampuni ya EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT walipoenda kutembelea kituo cha FARAJA
ORPHANS CHILDREN HOME….
|
WASANII WA MAIGIZO TOKA EMAGS WAKIELEKEA KITUO CHA FARAJA |
|
MSANII WA FILAMU TOKA EMAGS IBRAHIM JAMAL (KULIA) AKIWAVUSHA WATOTO KUELEKEA UWANJANI |
|
RODGERS(KUSHOTO) , ANNA (KATIKATI) NA MWIJAGE (KULIA) PAMOJA NA WATOTO WA KITUO CHA FARAJA |
|
PAULINE (ALIYEVAA T SHIRT NYEUPE) TOKA EMAGS AKIWA NA WATOTO WA KITUO CHA FARAJA |
|
WAIGIZAJI WA FILAMU TOKA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT NA WATOTO WA KITUO CHA FARAJA ORPHANS CHILDREN HOME |
|
WAIGIZAJI WA FILAMU TOKA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT NA WATOTO WA KITUO CHA FARAJA ORPHANS CHILDREN HOME |
|
WAIGIZAJI WA FILAMU TOKA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT NA WATOTO WA KITUO CHA FARAJA ORPHANS CHILDREN HOME |
|
WAIGIZAJI WA FILAMU TOKA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT NA WATOTO WA KITUO CHA FARAJA ORPHANS CHILDREN HOME |
|
WAIGIZAJI WA FILAMU TOKA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT WAKIFANYA DRAMA |
|
WAIGIZAJI WA FILAMU TOKA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT WAKIFANYA DRAMA |
No comments:
Post a Comment