WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Wednesday, February 6, 2013

BAADA YA KUWA KWENYE MAOVU KWA MUDA MREFU MSANII MAARUFU WA FILAMU TOKA ARUSHA PROFESSIONAL MOVIES AAMUA KUMRUDIA MUNGU

Msanii marufu kutoka Jijini Arusha katika tasnia ya filamu ambaye pia ni mwalimu wa sanaa katika vikundi mbalimbali ameamua kumrudia Mungu baada ya kutenda maovu kwa muda mrefu.

ABBY au KELVIN
Akizungumza na mwandishi wa habari hii msanii huyo alisema kua “ NIMEAMUA KUMRUDIA MUNGU BAADA YA KUONA MAMBO YA DUNIANI HAYAFAI NA HAYANA FAIDA KWA UPANDE WANGU”
Pia aliongeza kua “KAMA NI UZINZI NIMEFANYA HADI NIMECHOKA NA WANAWAKE TOFAUTI TOFAUTI HADI WENGINE NI WAKE ZA WATU, NIMEWADANGANYA WATU WENGI SANA LAKINI WENGI WAO NI WANAWAKE NA PIA NIMEFANYA MAMBO MENGI MABAYA ZAIDI YA HAYA”
Msanii huyo aliendelea kukiri kuwa “NILIWAHI KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA WASANII WENZANGU WENGI TU WA EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT NA PIA TULIVYOENDA TANGA MASHAALAH NILIPATA MTOTO WA KITANGA AITWAYE JOHARI TOKA KUNDI LA MAJUTO ARTS LILILO CHINI YA MSANII NGULI WA KOMEDI TANZANIA KING MAJUTO”
Msanii huyo wa filamu ambaye anafahamika kwa jina la ABBY kabla ya kubatizwa na kuokoka na kwa sasa anaitwa KELVIN baada ya kuokoka na kumrudia Mungu.
Alipo ulizwa na mwandishi wa habari hizi kuwa kwa sasa anasali kanisa gani, msanii huyo alisema “KWA SASA NASALI KATIKA KANISA LA BETHELI CHRISTIAN CENTER LILILOPO KIJENGE CHINI YA MCHUNGAJI ORAL SOSY, PIA NAIMBA KWAYA HAPO KANISANI KWANI NINA KIPAJI CHA KUIMBA PIA”
www.arushaprofessionalmovies.blogspot.com itaendelea kuwaleta habari za msanii huyo wa filamu namna anavyoendelea katika wokovu wake.

No comments:

Post a Comment