WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Wednesday, February 6, 2013

MSANII MAARUFU WA FILAMU ATELEKEZA MKE NA MTOTO


EVERYBODY
Habari zilizotufikia katika dawati letu la habari za uhakika kuwa msanii mmoja maarufu wa filamu hapa Jijini Arusha aliyetamba katika filamu tofauti tofauti alizozicheza kama muhusika mkuu ambazo ni MATEKA WA KIROHO, STANDARD 7, CHOZI LA YATIMA na mzigo mpya unaokuja toka STEPS ENTERTAINMENT uitwayo TEMPTETION OF MY WIFE pamoja na tamthilia ya HAIBA YA PENZI ambazo zimetengenezwa hapa hapa jijini Arusha na kampuni maarufu ya utengenezaji filamu EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT,
Habari hizi zinasema kuwa msanii huyu inasadikika kuwa alitelekeza familia yake baada ya kua na mahusiano na msanii mwenzake maarufu wa filamu hapa jijini Arusha.

COVER LA FILAMU YA MATEKA WA KIROHO
Inasemekana kuwa msanii huyo ambaye jina lake halisi ni JOSEPHAT HOREST na maarufu kwa jina la EVERYBODY alimwache mke na mtoto {MAMA CATHY}  na kuingia kwenye mahusiano na msanii mwenzake MWANAHAMISI MZIRAY maarufu kama MISHI.
Mtoa habari wetu aliendelea kusema kuwa mahusiano ya EVERYBODY na MISHI hayakudumu kwa muda mrefu kwani alimpa kibuti na kuvuta kifaa kingine kipya toka kundi moja la sanaa hapa jijini Arusha aitwaye NASRA ambaye kwa sasa ana mtoto na haijulikani ni mtoto wa nani na kwa sasa msanii EVERYBODY amemlazimisha NASRA kumuachisha mtoto kunyonya ili aendelee kuponda raha kama kawa.

COVER LA FILAMU YA STANDARD 7
Kwa upande mwingine mwandishi wetu alimua kujikiingiza mtaani na kumtafuta mke wa EVERYBODY ambaye ni MAMA CATHY na kupiga nae story mbili tatu juu ya sakata hili ndipo yakazuka mengine ambayo tulikua hatuyafahamu ambayo ni
“Mimi na mume wangu kwa kweli tuligombana baada ya yeye kuwa star wa filamu kwani hapo nyuma tulikua tunaishi kwa amani hadi tulipofanikiwa kumpata mtoto wetu huyu {akimwonyesha cathy}, kwa sasa hatuna mahusiano mazuri kwani kuna kipindi tulifikishana mpaka USTAWI WA JAMII kwani yeye alikua haleti pesa ya matumizi ya mtoto”
Baada ya kupata habari hizi mwandishi wetu aliamua kumtafuta EVERYBODY lakini hakupatikana na alipotafutwa kwenye simu nayo iliita pasipo kupokelewa.
www.arushaprofessionalmovies.blogspot.com itawaletea interview maalumu na msanii EVERYBODY baada ya kumpata.

??????????????????????????

No comments:

Post a Comment