NDUGU AWADHI NGOMA MKURUGENZI - KUNDI LA SANAA LA WATOTO WA SIMBA |
Kikundi
cha sanaa cha ngoma na maigizo cha WATOTO WA SIMBA chenye makazi yake Jijini
Arusha kimegomea ofa ya safari yao ya kwenda kufanya tamasha katika Jimbo la
GOHA nchini INDIA.
Akizungumza
na mwandishi wetu wa www.arushaprofessionalmovies.blogspot.com
katika ofisi zetu ndugu AWADHI RAMADHANI MWINYI maarufu kwa jina la AWADHI
NGOMA ambaye ni Mkurugenzi wa kundi hilo alisema kuwa “Tumeona tusiende kwenye
tamasha hilo nchini INDIA kutokana na promota wetu kutupa maslahi madogo, ila
tunashukuru baadhi ya wasanii wamepata passport za kusafiria ili ikitokea tena
safari ya nje tunaweza kwenda bila usumbufu wowote”
NDUGU AWADHI AKIONGEA NA MHARIRI WETU KATIKA OFISI ZA ARUSHA PROFESSIONAL MOVIES |
Bwana
AWADHI aliendelea kusema “Tulioneshwa barua ya mwaliko wa kufanya tamasha hilo
ambapo ilikua tunatakiwa kulipwa dola 1200, lakini malipo hayo yalikua
yanakatwa na sisi kubaki na dola 400 kwa mwezi na chakula cha jioni walikua
wanajitegemea wenyewe”
Safari
yao ya kwenda nchini INDIA ilikua waende tarehe 5 march na walikua wanakaa kwa
muda wa miezi sita, na alitoa ushauri kwa mapromota kuwa “Mapromota wasipende
kujifikiria wenyewe waweke mbele maslahi ya wasanii halafu ndio yao ifuate
kwani kundi lao lina jumla ya wasanii nane”
No comments:
Post a Comment