WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Wednesday, February 6, 2013

MTANGAZAJI MAARUFU WA SIBUKA TV NA MPIGA PICHA MAARUFU WA CLOUDS TV WAWASUSA WAPENZI WAO WAKATI WA KUSHEHEREKEA SIKU ZAO ZA KUZALIWA


www.arushaprofessionalmovies.blogspot.com kama kawaida inafuatilia habari zinazowahusu wasanii wa filamu hapa Jijini Arusha..
Weekend hii tuliingia mtaani na kukutana na malalamiko toka kwa wanadada wawili tofauti wakiwalaumu wapenzi wao kuwasusa katika kusheherekea siku zao za kuzaliwa..

DEO G
 Hii imetokea tarehe 3/2/2013 majira ya mchana ambapo Mtangazaji maarufu wa SIBUKA TV ambaye ana host show ya MASHARIKI HITS HIGH REQUEST ndugu ARNOLD RWEYEMAMU a.k.a DIZZO MAN DILUNGA pamoja na mpiga picha maarufu wa habari wa chombo cha CLOUDS TV hapa Jijini Arusha DEOKGRATIUS KASSAMIA a.k.a DEO G ambao pia ni wasanii wa filamu kwani walishawahi kucheza filamu nyingi ambazo ni MATEKA WA KIROHO , CHOZI LA YATIMA na tamthilia kali ya HAIBA YA PENZI..
Wanaume hawa inasemekana mnamo tarehe 3/2/2013 walionekana maeneo ya NGURDOTO wakiwa na mademu wengine tofauti na wapenzi wao wanaofahamika,
Hayo yalisemwa na wapenzi wa wanaume hao ambao ni DELPHINE NDOSSY pamoja na SOPHIA JUSTINE waliyasema hayo baada ya kuandaa zawadi za kuwapa wapenzi wao na siku ilipofika ya kusheherekea siku zao za kuzaliwa wapenzi wao hawakuonekana na inasemekana walionekana maeneo ya ngurdoto wakijirusha na wanawake wengine.
Waliendelea kusema kuwa “zawadi zetu tulizowanunulia ili kuwapa wapenzi wetu tuliamua kuwapa ndugu, jamaa na marafiki kwani inaonekana kuwa wsisi hatuna thamani mioyoni na maishani mwao”

DIZZO MAN DILUNGA
 Kwa upande wao DIZZO MAN DILUNGA na DEO G wao pia walifunguka kuwa “siku hiyo kwa kweli tulikua tuko Ngurdoto lakini hatukua na wasichana wala hatukujirusha ila tulikua tunafuatilia habari kwani kulikua na mkutano wa viongozi wanchi mbalimbali hivyo tuliamua kusheherekea siku hiyo tukiwa kazini”
Lakini kwa habari za uhakika toka www.arushaprofessionalmovies.blogspot.com ni kuwa siku hiyo ya Jumapili ya tarehe 3/2/2013 hakukua na kikao chochote hapo Ngurdoto hivyo kuonekana kuwa ni kweli walikua wanajirusha na wapenzi wengine na kuwaacha solemba wapenzi wao wanaofahamika na watu wote.

No comments:

Post a Comment