WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Saturday, February 23, 2013

SAKATA LA KUMPA MIMBA MTOTO MWENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 YAIBUA MAPYA






Lile sakata la kumpa msichana mdogo mwenye umri chini ya miaka 18 laendelea kuibua mapya baada ya msanii anayedaiwa kufanya unyama huo kuibuka na kukanusha vikali kuhusika na jambo hilo.

Msanii huyo ambaye alifika katika ofisi za Arusha Professional Movies amekanusha vikali kwa kusema kilichoandikwa kililenga kumchafulia jina na haiba yake katika jamii.

“Kilichoandikwa kililenga kunichafua na kunidhalilisha” alisema msanii huyo huku akionekana mwenye jazba
Msanii huyo anayefahamika kwa jina la MASS B anayedaiwa kuwa ni msanii katika kikundi cha sanaa cha AGESTA kilichopo Jijini Arusha alikua ameambatana na baadhi ya viongozi wa kundi hilo, amesema katika maisha yake hatarajii kutoka kwa njia ya skendo kama wasanii wengine.
“Mimi katika maisha yangu sitarajii kutoka kwa skendo na ndio maana nafanya kazi zangu za sanaa kwa juhudi na kujituma”alisema msanii huyo.

Aidha ameongeza kwamba hivi sasa yeye ameajiriwa na shirika linaloshughulika na watoto hivyo kitendo cha kumuandika hivyo kinaweza kuhatarisha kibarua chake na hivyo kumkosesha riziki.

“Kwa kweli sujafurahishwa na habari hizo kwani zinaweza kuniharibia kibarua changu” alisema MASS B huku akiwa na sura ya huzuni.

Hata hivyo msanii huyo aliweza kuthibitisha kuwa alimpa binti huyo mimba lakini hana miaka chini ya kumi na nane kama ilivyodaiwa hapo awali na kwa sasa wanaishi pamoja.

Aidha kwa upande wake kiongozi wa kundi hilo aliyeambatana na msanii huyo aliyefahamika kwa jina moja la CHRISS  alisema “Sisi AGESTA kwa sasa tumejiwekea heshima mbele ya mkuu wa Mkoa pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, hivyo tunaomba sana, kikundi chetu kisihusishwe kwa namna yeyote ile na masuala binafsi ya msanii mmoja mmoja. Kikundi kisihusishwe kutokana na heshima yetu kwa viongozi hao”

Arusha professional movies inawatakia kila la kheri kundi hili la AGESTA katika kazi zao za sanaa.

No comments:

Post a Comment