WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Monday, February 18, 2013

WAFANYAKAZI WA RADIO FIVE ARUSHA WAPIGWA NA KUGARAGAZWA NA WASANII WA FILAMU



Hiki ni kipigo ambacho hakijawahi kutokea kwani wasanii wa filamu toka kampuni ya EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT waliweza kuwachapa na kuwaadabisha hadharani bila woga wowote mbele ya wasikilizaji wao wafanyakazi wa RADIO FIVE ARUSHA kwa kuwafunga goli 6 kwa 1.

Mchezo huo wa aina yake ulifanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa GENERAL TYRE Jijini Arusha ulishuhudia RADIO FIVE ARUSHA ikipokea kipigo heavy toka kwa wasanii wa filamu wa kampuni ya EMAGS VIDEO ENTERTAINMENT.
Magoli hayo yalifungwa na wachezaji tofauti. 

wakiongozwa na team captain RODGERS ISRAEL NELSON aliyefungua pazia la kufunga magoli kwa timu ya waigizaji wa filamu  mnamo dakika ya tatu tu ya mchezo, goli la pili lilifungwa na IBRAHIM JAMAL kiungo mchezeshaji, goli la tatu lilifungwa na winga machachari na mfupi kuliko wote ABBY CARTER, goli la nne na la tano lilifungwa na mshambuliaji hatari asiyecheka na nyavu SEVERINUS MWIJAGE Jr na goli la mwisho lilifungwa na kiungo mshambuliaji MAULIDI huku RADIO FIVE ARUSHA wakijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya tisini ya mchezo lililofungwa na MENEJA wa RADIO FIVE ARUSHA ndugu JIMMY.

Hata hivyo baada ya kuchapwa magoli matatu ya mwanzo RADIO FIVE ARUSHA walianza kulaumiana na mchezaji wao SEMIO SONYO alianza kugoma kucheza kwa madai ya kutoelewana na mchezaji mwenzake lakini wachezaji wenzake wakasema ni kawaida yake kwani ndivyo anavyotafuta sifa..

Mechi yenyewe ilikua hivi………………..


















No comments:

Post a Comment