WASANII WANAHITAJIKA

EMAGS

Friday, February 22, 2013

MSANII AWALIZA WENZAKE



           awataadharisha mabinti kukaa chonjo na waume zao.
MAURINE KATIKA POZI
 Ule Msemo wakula kutokana na ulefu wa kamba yako umejidhihirisha kwa msichana mmoja ambaye ameamua kuachana na kazi yake ya usekretari na kujikita katika tasnia ya filamu akiamini upande huo kuwa ndo sehemu rahisi ya mabinti kutokea ndani ya bongo land.

Msichana huyo ambaye jina lake ni adimu kulijua haswa baada ya kujipachika majina tofauti katika kila jambo afanyalo kwa lengo lakutozoeleka,ambapo baadhi ya majina atumiayo ni Maureen au Happy na hivi karibuni akijibadili kabisa jinsia na kujiita Daddy.

Aidha baada ya kujikita katika tasnia ya filamu mrembo huyo amejikuta katika skendo nzito baada ya kudaiwa kuvuruga mahusiano ya kimapenzi  ya msanii mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Jane ambaye licha ya usanii ni msusi katika saloon moja maarufu mitaa ya Ilboru (jina tunalihifadhi)nakujikuta wakirumbana kila wanapokutana na kuacha maswali kwa wasanii na jamii kwa ujumla.

Arusha professional ilitililishiwa mpambano mkali uliojitokeza katika saluni hiyo hivi karibuni,ambapo wasichana hao walitaka kuzichapa kavukavu mbele ya hadhira  bila hata aibu wakidaiwa kumgombania kipoba huyo wa kitaa ambaye ni dereva mkongwe wa kampuni ya utalii jijini hapa ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi.

Hata hivyo walionekana kuogopana na kuishia kulushiana maneno ya kejeli na kashfa za kuvuana nguo,kwa kile kilichoonekana kila mmoja kujinadi kulala na njemba hiyo,kwa upande wa Jane “mimi ni mrembo sana na jamaa anajua mziki wangu tuwapo faragha,na pia ananipenda sana kwa muda mrefu ,wewe nikama wajiuza tu kwani ni wajuzi,najua ni shida zako za kodi halooooo”  kama haitoshi Happy nae akajibu mapigo kwa kijembe cha moto.

“we sema yote lakini ujue kuwa umechuja,angalia nilivyo bado mbichi si wewe uliyeingia leba mara kibao na kukongoroka mimi jana tu nimelala nae na kama haitoshi jumamosi nahamia kabisaaaa,kama vipi andamana mimi ndo mtoto wakichaga utaisoma namba mjini hapa kila mbuzi ula kwa urefu wa kamba yake”

Licha ya ugomvi huo Maureen au Happy amezidi kukubwa na jinamizi la uhalibifu baada ya kuonekana na mchumba wa msanii mwenzake ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha televisheni jijini Dar,na kuonyesha mahaba bila woga wala haya ,blog hii ilimpigia simu nakujibu kuwa asisumbuliwe kwani alikuwa darasani ,hata hivyo tutakuletea muendelezo wake kesho.

MAURINE NA MUME WA MTU
Arusha professional movie inalaani kitendo hiki nakuwaomba wasanii hao kusuluhisha nakuachana na tabia hizo kwani si usanii bali kuchafua tasnia hii ambayo bado changa.

No comments:

Post a Comment